Sura zenye furaha: Lionel Messi akisaini mkataba mpya mbele ya Rais wa Barcelona Josep Maria Bartomeu |
Lionel
Messi ameweka saini ya kuongezea mkatana wake na klabu yake ya
Barcelona mkataba ambao utamfanya kuwa mchezaji anayelipwa pesa nyingi
zaidi dunia ambapo atakuwa akipokea pauni milioni £16.3 kwa mwaka.
Mshambuliaji huyo wa Barcelona ameonekana akiwa katika picha na Rais wa klabu hiyo Josep Maria Bartomeu
akisaini mktaba wake mpya ikiwa ni siku mbili baada ya msimu wa ligi kuu ya nchini Hispania La Liga kumalizika.
Messi sasa anakuwa ni zaidi ya nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo anayelipwa (£15m) kwa mwaka.
Lionel Messi amekubali mkataba mpya
Mkataba
wa awali wa Messi umefanyiwa ukarabati kiasi kwamba posho yake hiyo
ukiachana na bonasi utakuwa ukifanyiwa marekebisho kila mwaka wa mkataba
mpya.
Hiyo
maana yake ni kwamba Messi atakuwa akipokea pauni milini £16.3 msimu
ujao lakini endapo kama atashinda ligi ya mabingwa bonasi yake
itaongezwa na hivyo jumla yake itakuwa ni malipo mapya kuelekea msimu
utakao fuata.
Kiwango
cha pesa cha uvunjaji wa mkataba cha pauni milioni £250 kimesalia hivy,
na hiyo inaweka milango wazi kwa vilabu vyenye njaa ya kupata huduma ya
Messi kama vile
Manchester City au Paris Saint-Germain kuweka fedha mezani endapo
watafikia kiwango hicho ingawa vita ya mpango wa matumizi mabaya ya
fedha FFA( Financial Fair Play ) ikionekana kuwa tishio.
Taarifa ya Catalans iliyotolewa Ijumaa iliyopita imesomeka
'FC Barcelona imefikia makubaliano ya kufanyia mabadiliko vifungu vya mkataba wa Leo
Messi ndani ya klabu, mabadiliko hayo na zoezi la kusainiwa mkataba litafanyika siku chache zijazo'
No comments:
Post a Comment