Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, March 10, 2014

TFF YAIOMBA RADHI SERIKALI, UHARIBIFU VITI TAIFA: WANAOFANYA VUFO, UHARIBIFU VIWANJANI KUKIONA CHA MOTO!!

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) tunalaani vikali fujo na uhabirifu wa mali unaofanywa na washabiki viwanjani wakati mechi mbalimbali zikiwemo zile za kimataifa na ligi za hapa nchini. Tunaiomba radhi Serikali kwa uharibifu wa viti uliotokea kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga ya Tanzania na Al Ahly ya Misri iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Uharibifu huo wa viti umesababisha hasara ya sh. milioni 15 kwa wamiliki wa uwanja huo ambao ni Serikali.TFF tutalipa fedha hizo kwa Serikali kutokana na uharibifu huo.Tunaendelea kuchunguza tukio hilo, huku tukijiandaa kutoa adhabu kwa klabu na washabiki husika kulingana na kanuni zetu. Adhabu itakuwa kali ili iwe fundisho kwa wengine.Kwa mujibu wa Serikali, viti kumi viling’olewa na kutupwa ovyo ovyo uwanjani wakati vingine 40 viliathirika kutokana na vurugu za watazamaji hao.Tumebeba dhamana ya kulipa uharibifu huo kwa vile TFF ndiyo wenye dhamana ya kusimamia mechi za kimataifa, na ndiyo tulioomba idhidi ya kutumia uwanja huo.Kwa vile sasa baadhi ya washabiki, wapenzi na wanachama wa klabu mbalimbali nchini wanataka kufanya suala la uharibifu kuwa la kawaida na mazoea, Serikali inakusudia kuchukua mapato yote ya mchezo husika endapo kutatokea uharibifu.Hivi viti ni baadhi viling'olewa wakati wa mtanange wa Simba na Kagera Sugar kipindi cha nyuma kidogoPia kuruhusu uwanja kutumiwa bila watazamaji kwa baadhi ya mechi, na kutoruhusu uwanja huo kutotumika kabisa kwa baadhi ya mechi.

Boniface Wambura Mgoyo
Media and Communications Officer
Tanzania Football Federation (TFF)

No comments:

Post a Comment