Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, March 30, 2014

ARSENAL 1 v MANCHESTER CITY 1, HAKUNA MBABE, FLAMINI AISAWAZISHA GUNNERS NA KUTOKA SARE EMIRATES!

Arsenal leo wakiwa kwao Emirates kucheza mechi ligi kuu England na Manchester City wametoka nyuma ya bao moja na kusawazisha bao kwa kufanya 1-1. Manchester City ndio walikuwa wa kwanza kuandika bao lao katika kipindi cha kwanza Dakika ya 18 kupitia mchezaji wake David Silva Baada ya City kufanya Shamulizi kwenye lango la Arsenal. Kipindi cha pili Dakika ya 53 Arsenal walisawazisha bao baada ya kufanya nao mashambulizi makali kwenye lango la City, Bao likifungwa na Mathieu Flamini baada ya kupewa krosi safi na Lukas Podolski. Sare hii ni ya Pili kwa timu ya Arsenal baada ya mechi ya katikati ya wiki kutoka sare na timu ya Swansea City kwa sare ya 2-2 na wakijifunga wao kushinikiza sare hiyo, Leo hii tena wametoka sare na kugawana pointi moja moja na Manchester City. Mechi inayofuata kwa Arsenal ni Everton ambao pia wako chini yao wakiwa na pointi 57. Sare hii ya Arsenal pia inawapatia pointi 67 na Arsenal pointi 64.
Pia Matokeo haya yameifanya Chelsea ibakie kileleni ikiwa Pointi 1 mbele ya Liverpool ambao Jumapili wanacheza na Tottenham Uwanjani Anfield huku City wakiwa Nafasi ya 3 na Arsenal Nafasi ya 4.Kocha wa City akiwapa maelekezo wachezaji wake leo kwenye uwanja wa EmiratesFlamini akipeta na kushangilia bao lake kipindi cha pili dakika ya 53.Lucas akiachia shuti na Kipa wa City kuliokoa...Bao..1-1Yaya Toure akiendeshaVuta nikuvute!Patashika kwenye lango la Arsenal
Kipa wa Arsenal Wojciech Szczesny akiokoa mpira dhidi ya Fernadinho wa CityChupu chupu, Martin Demichelis na Tomas Rosicky wazipange!Na huyu tena!
Nani zaidi ?Flamini akijiingiza mwenyewe kwa Silva..Alvaro Negredo akiendeshaBacary Sagna akiwa hoi chini

No comments:

Post a Comment