TIMU ya
Taifa ya Wanawake(Twiga Stars) imetolewa katika mashindano ya raundi ya kwanza
kuwania kufuzu fainali za Mataifa Afrika kwa wanawake baada ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi
ya Shepolopolo ya Zambia katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex
Chamazi, Dar es Salaam.
Katika mechi
ya kwanza iliyochezwa nchini Zambia Twiga Stars ilifungwa mchezo huo kwa mabao
2-1 hivyo imetolewa kwa jumla ya mabao
3-2.
Katika mechi
hiyo iliyokuwa na ushindani mkali, Twiga Stars ndio walioanza kupata bao la
kuongoza dakika ya 39 kupitia kwa Asha Rashid akiwa ameunganishiwa
pasi kutoka kwa Vumilia Maarifa.
Ushindi huo
uliipeka Twiga Stars hadi mapumziko ya kipindi cha kwanza bila kuwapa nafasi
Shepolopolo waliokuwa wakijitahidi kwa kila namna ili kusawazisha.
Baada ya
mapumziko timu zote zilikuwa na ushindani mkali lakini dakika ya 65 Kocha
Rogasian Kaijage alifanya mabadiliko katika kikosi chake cha Twiga Stars kwa
kumtoa Shelder Boniface na kumwingiza Fatuma Mustafa lakini bado haikusaidia.
Mnamo dakika
ya 80 Shepolopolo walifanikiwa kusawazisha bao la kwanza kupitia kwa Suzan
Banda baada ya mchezaji wa Twiga Stars Evelyn Sekikubo kumfanyia madhambi Mzambia Hellen Mubanga katika eneo la hatari.
Bao hilo
lilipigwa moja kwa moja na kuingia golini, baada ya Kipa Fatuma Omar konekana
kukaa nyuma ya mabeki waliokuwa wamemziba bila kuona mpira uliokuwa ukigongwa.
Aidha,
dakika ya 86 Kocha Kaijage alifanya tena mabadiliko kwa kumtoa Amina Ally na
kumwingiza Zena Khamis ili kuleta matunda, lakini ushindani ulikuwa mkali kila
upande.
Pamoja na
hayo yote, Twiga Stars ilipoteza nafasi nyingi za kufunga ambapo dakika ya 5,
7, 13, 20 walikuwa wakipiga mipira ikipaa na kutoka nje.
Kutokana na
kupoteza mchezo huo, Twiga Stars watapumzika hadi mwakani katika michuano
mingine.
No comments:
Post a Comment