MENEJA
wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amesema kiungo wake Mesut Ozil bado
anatafunwa na dhambi ya kukosa penati katika mchezo dhidi ya Bayern
Munich. Kiungo aliyevunja rekodi katika usajili wake alipata penati ya
mapema katika mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya lakini alikosa
kwa kumpigia moja kwa moja kipa wa Bayern Manuel Neuer. Akihojiwa
Wenger amesema kwasasa wanamuacha asahau yaliyotokea kwasababu yamepita
masaa 48 toka akose penati hivyo ni muda mfupi sana. Wenger amesema ana
mifano ya wachezaji waliopitia wakati kama wa Ozil akiwemo Dennis
Bergkamp ambaye alikosa penati dhidi ya Manchester United mwaka 1999
katika nusu fainali ya Kombe la FA na hakutaka kupiga penati baada ya
hapo lakini leo ana sanamu lake nje ya uwanja wao.Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger
Ozil juzi alikosa penati!
Mesut Ozil akiachia shuti njaa na kudakwa na kipa Never juzi usiku
No comments:
Post a Comment