Ligi
Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaingia raundi ya 16 Februari 5 mwaka huu kwa mechi tano huku Mtibwa Sugar ikiikaribisha
Simba kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Kiingilio
katika mechi hiyo ambayo itakuwa ya kwanza kuchezwa kwenye uwanja huo wenye
uwezo wa kuchukua watazamaji 10,000 tangu uanze mzunguko wa pili wa VPL kitakuwa
sh. 5,000. Jonisia Rukyaa kutoka Bukoba ndiye atakayechezesha mechi hiyo.
Mechi
nyingine za ligi hiyo ni Tanzania Prisons vs Coastal Union (Sokoine, Mbeya),
Mgambo Shooting vs Ruvu Shooting (Mkwakwani, Tanga), Rhino Rangers vs Oljoro
JKT (Ali Hassan Mwinyi, Tabora) na JKT Ruvu vs Ashanti United (Chamazi, Dar es
Salaam).
No comments:
Post a Comment