Fomu za wagombea
kwa ajili ya uchaguzi wa Kamati mpya ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa
Habari za Michezo Tanzania (TASWA) utakaofanyika Machi 2, 2014 jijini Dar es Salaam
zimeanza kutolewa leo (Februari 24 mwaka huu).
Mwisho wa kuchukua
na kurudisha fomu hizo zinazotolewa Idara ya Habari (Maelezo) ni Alhamisi
(Februari 27 mwaka huu) saa 9 alasiri.
Ada kwa wagombea
wa nafasi za Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi,
Mhazini na Mhazini Msaidizi ni sh. 50,000 kwa fomu. Nafasi za wajumbe wa Kamati
ya Utendaji fomu zinapatikana kwa sh. 20,000.
Kwa mujibu wa
Ibara ya 21(e)(i), sifa ya elimu kwa wanaowania nafasi za Mwenyekiti hadi
Katibu Msaidizi ni diploma au digrii ya uandishi wa habari. Kwa nafasi nyingine
kwa mujibu wa Ibara ya 21(e)(ii) ni cheti cha ngazi yoyote katika uandishi wa
habari.
Tunawahimiza
wanachama wa TASWA kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu ili waweze kuwania nafasi
hizo.
Boniface Wambura
MWENYEKITI KAMATI YA UCHAGUZI TASWA
Februari 24, 2014
Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment