Waombaji 27 kati
ya 28 wamerejesha fomu kuomba kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwenye
uchaguzi wa Kamati mpya ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo
Tanzania (TASWA) utakaofanyika Machi 2, 2014 jijini Dar es Salaam.
Mwisho wa kuchukua
na kurudisha fomu hizo ilikuwa leo Alhamisi (Februari 27 mwaka huu) saa 9
alasiri.
Waliorejesha kwa
nafasi ya ujumbe ni Arone Benedict Mpanduka, Elizabeth Rashid Mayemba, Emmanuel
Augustino Muga, Hassan Maulid Bumbuli, Ibrahim Mkomwa Bakari, Masau Kuliga
Bwire, Mbozi Ernest Katala, Mroki Timothy Mroki, Mussa Juma, Mwani Omary
Nyangassa, Rehure Richard Nyaulawa, Salum Amiri Jaba, Tullo Stephen Chambo na
Urick Chacha Maginga.
Mhazini Msaidizi
ni Elius John Kambili, Zena Suleiman Chande wakati Mhazini Mkuu ni Shija
Richard Shija na Mohamed Salim Mkangara.
Katibu Msaidizi ni
Alfred Lucas Mapunda, Grace Aloyce Hoka na Ptarick Raymond Nyembera. Katibu
Mkuu ni Amir Ally Mhando pekee.
Waombaji nafasi ya
Makamu Mwenyekiti ni Egbert Emmanuel Mkoko, Maulid Baraka Kitenge na Mohamed
Omary Masenga. Waliojitosa kwenye nafasi ya Mwenyekiti ni George John
Ishabairu, Juma Abbas Pinto.
Ni Shaffih Kajuna
Dauda pekee ambaye hakurejesha fomu. Dauda alichukua fomu ya kuwania uenyekiti.
Boniface Wambura
MWENYEKITI KAMATI YA UCHAGUZI TASWA
Februari 27, 2014
Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment