TIMU ya mchezo wa pete ya mkoa wa Temeke imefanikiwa kutetea
ubingwa wake wa mashindano ya Taifa Cup, baada ya kuifungaMorogoro mabao 52-38
kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Temeke walianza kuliandama lango la Morogoro tangu robo ya kwanza ya mchezo kwani
walikwenda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 15 na Morogoro wakiwa na mabao 7 pia Temeke walizidi kung’aa
kwenye robo ya pili baada ya kuifunga Morogoro
mabao 12 kwa 8.
Kwenye robo ya tatu Morogoro
walizidi kupotea na kujikuta
wakifungwa mabao 14 kwa 10 na robo ya nne ya kukamilisha mchezo Morogoro
walizinduka na kuifunga Temeke mabao 17
kwa 14.
Morogoro hawatamsahau GS wa Temeke Mwanaidi Hassan kwani
ndiye alikuwa mwiba mchungu kwa kutumbukiza mabao mengi katika mchezo wao.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mbunge wa Temeke, Abbas
Mtemvu alisema kuwa Temeke wanafanya vizuri na watatetea ubingwa wake kutokana
na maandalizi mazuri walioyafanya
Naye Mwenyekiti wa
Chama cha Netbali (CHANETA) Anna Kibira alimpongeza na wafadhili waliojitoa
kukisaidia Chama chake na kuomba wadau wengine kujitokeza kuisaidia timu ya
Taifa “Kilimanjaro Queens” inayokwenda kwenye mashindano ya Mapainduzi.
No comments:
Post a Comment