Hata hivyo sekretarieti ya TASWA imekubaliana kusogeza mbele
muda wa kulipia ada kwa wanachama hadi Jumanne Februari 4 mwaka huu, badala ya
Ijumaa Januari 31, 2014 iliyokuwa imepangwa awali, lengo likiwa ni kuwezesha
wanachama wengi zaidi kulipia ada zao ili waweze kushiriki uchaguzi huo.
Wanachama wote walioshiriki uchaguzi wa mwaka 2007 ama 2010
au Mkutano Mkuu wa mwaka 2012 wana sifa ya kushiriki uchaguzi huo wanachotakiwa
kufanya ni kulipia ada zao kuanzia mwaka 2011.
Malipo yafanywe kwa Mhazini Msaidizi, Mohammed Mkangara,
0658-123082 na hakuna mwanachama mpya atakayekubaliwa kujiunga na chama kwa
sasa mpaka baada ya Uchaguzi Mkuu.
Nawasisitiza wanachama kuhakikisha wanatumia vizuri muda
uliobaki kwa kulipia ada zao ili waweze kushiriki mkutano huo. Kamati ya
Uchaguzi ya TASWA inatarajiwa kukutana Jumatatu ijayo kuzungumzia mambo
mbalimbali yahusiyo uchaguzi huo.
Nawasilisha.
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA
29/01/2014.
No comments:
Post a Comment