Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, January 4, 2014

SIMBA YATOKA SARE NA KCC MAPINDUZI CUP

Na Mahmoud Zubeiry, Zanzibar
SIMBA SC imegawana pointi na KCC ya Uganda baada ya sare ya bila kufungana katika mchezo wa Kundi B, Kombe la Mapinduzi usiku huu Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Kwa ujumla timu zote zilitoshana nguvu na maarifa kwa dakika zote 90 za mchezo huo, huku makipa wote, Ivo Mapunda wa Simba na Magoola Omar wa KCC wakistahili sifa kwa kuokoa michomo mingi ya hatari.
Mabeki wa KCC walimdhibiti vizuri winga machachari wa Simba SC, Ramadhani Yahya Singano ‘Messi’ leo, wakati pia beki Mkenya, Donald Mosoti Omwanwa aliiongoza vyema safu ya ulinzi ya Simba SC. 
Kipa wa KCC, Magoola Omar akiruka juu kupangua mpira kichwani kwa mshambuliaji wa Simba, Betram Mombeki jioni hii Uwanja wa Amaan

Matokeo hayo yanazifanya Simba SC na KCC ziendelee kukabana kileleni, kila timu ikiwa na pointi nne baada ya kucheza mechi mbili.
Mapema jioni katika mchezo wa kwanza wa kundi hilo, wenyeji KMKM nao walitoshana nguvu na AFC Leopard ya Kenya kwa sare ya 0-0 pia.
Mechi za Kundi B zitahitimishwa Januari 5, kwa Simba kumenyana na KMKM na KCC na Leopard.
Michuano hiyo itaendelea kesho kwa mechi za Kundi C, Ashanti ikimenyana na Spice Stars na Azam FC na Tusker ya Kenya Uwanja wa Amaan, wakati Uwanja wa Gombani, Pemba Clove Stars itamenyana na URA ya Uganda na Mbeya City na Chuoni.
Katika mchezo wa leo, kikosi cha Simba SC kilikuwa; Ivo Mapunda, Haruna Shamte, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Donald Mosoti, Joseph Owino, Jonas Mkude, Ramadhani Singano/Zahor Pazi dk89, Amri Kiemba/Said Ndemla dk50, Amisi Tambwe/Betram Mombeki dk67, Uhuru Suleiman/Ramadhani Chombo dk48 na Haroun Chanongo/Edward Christopher dk78. 
KCC; Magoola Omar, Saki Mpima, Kavuma Habibu, Kawooya Fahad, Kiiza Ibrahim, Senkumba Hakim, Waswa Herman, Masiko Tom, Tony Odur, Stephen Bengo/Gadafi Kiwanuka dk 58 na Wadri William.  

Winga machachariwa Simba SC, Ramadhani Singano 'Messi' akiruka guu la kipa wa KCC ya Uganda, Magoola Omar katika mchezo wa Kundi B Kombe la Mapinduzi jana Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana.
Beki wa KCC akimdhibiti Messi
Haroun Chanongo akiwatoka wachezaji wa KCC pembeni kushoto
Beki wa KCC akiondosha mpira hatarini dhidi ya mshambuliaji wa Simba, Amisi Tambwe
Messi alihaha Uwanja mzima jana, lakini wapi
Nafasi pekee nzuri ya Simba SC kupata bao aliipata Messi, lakini pamoja na kuwatoka vizuri mabeki akakwama kwa kipa Magoola Omar
Messi alijaribu kumpiga chenga kipa huyo, lakini Magoola akaupiga mpira ukaenda nje na Messi akapitiliza
Stephen Bengo wa KCC kushoto akipambana na viungo wa Simba SC
Haroun Chanongo kulia akitafuta maarifa ya kumpita beki wa KCC
Jonas Mkude alijaribu kupiga shuti la mbali, lakini likapaa juu kidogo ya lango
Betram Mombeki wa Simba SC akimtoka beki wa KCC
Kikosi cha Simba SC jana
Kikosi cha KCC
Wazee wa benchi; Wachezaji wa akina wa Simba SC, kutoka kulia ni Zahor Pazi, Abdulhalim Humud 'Gaucho', Kaze Gilbert chini na Yaw Berko 

No comments:

Post a Comment