-WAGOMBEA KOCHA BORA: SIR ALEX FERGUSON, JUPP HEYNCKES & JURGEN KLOPP!
-WAGOMBEA KINAMAMA: MARTA, ABBY WAMBACH & NADINE ANGERER!
-MANDELA, EUSEBIO KUPEWA HESHIMA MAALUM KWENYE HAFLA!!
Wachezaji hao watatu walifuzu kuingia Fainali toka Listi ya Wagombea 23 na Mshindi kati yao atatangazwa kesho Januari 13 katika Hafla maalum.
Washindi wa Tuzo hizi hupatikana kutokana na Kura za Makocha na Manahodha wa Timu za Taifa Wanachama wa FIFA pamoja na Wawakilishi wa Wanahabari toka Dunia nzima wanaoteuliwa na Jarida la Soka la Ufaransa France Football.
Kwa upande wa Kinamama, Wagombea wa Tuzo ya Mchezaji Bora ni Nadine Angerer (Germany), Marta (Brazil) na Abby Wambach (USA).
-MANDELA, EUSEBIO KUPEWA HESHIMA MAALUM KWENYE HAFLA!!
JUMATATU
Usiku, kuanzia Saa 1 na Nusu, huko Kongresshaus, Zurich, Nchini
Switzerland, mmoja kati ya Cristiano Ronaldo, Franck Ribery na Lionel
Messi ndio atatwaa Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani, 2013 Ballon d'Or.
Wachezaji hao watatu walifuzu kuingia Fainali toka Listi ya Wagombea 23 na Mshindi kati yao atatangazwa kesho Januari 13 katika Hafla maalum.
Washindi wa Tuzo hizi hupatikana kutokana na Kura za Makocha na Manahodha wa Timu za Taifa Wanachama wa FIFA pamoja na Wawakilishi wa Wanahabari toka Dunia nzima wanaoteuliwa na Jarida la Soka la Ufaransa France Football.
Kwa upande wa Kinamama, Wagombea wa Tuzo ya Mchezaji Bora ni Nadine Angerer (Germany), Marta (Brazil) na Abby Wambach (USA).
Kocha
Bora atachaguliwa kutoka Kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex
Ferguson, Kocha wa zamani wa Munich Jupp Heynckes na yule wa Borussia
Dortmund, Jurgen Klopp.
France Football ndio walioanzisha Ballon
d'Or Mwaka 1956 ili kumpata Mchezaji Bora Ulaya na Staa wa England,
Stanley Matthews, ndie alikuwa Mshindi wa Kwanza.
Mwaka 2007, Ballon d'Or iligeuka kuwa
Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani na kuanzia Mwaka 2010 ikawa FIFA Ballon
d'Or na Mshindi wake ni Messi tangu wakati huo.
Safai hii, baada ya kuitwaa Ballon d'Or
Mwaka 2008 akiwa na Manchester United, Cristiano Ronaldo, ndie
anaetegemewa kumpiku Messi ambae ameitwaa mara 4 mfulizo hadi 2012.
Wakati Ribery akitegemea mafanikio yake
na Klabu yake Bayern Munich yatamfanya afuzu, Ronaldo anategemea sana
Rekodi yake binafsi ya kupiga Bao nyingi ndio itampa Tuzo hiyo.
Na
hilo linampa nguvu Ronaldo kwani Tuzo hii ni ya Mchezaji binafsi na si
Timu na Goli zake 66 katika Mechi 56 kwa Klabu yake na Nchi yake kwa
Mwaka 2013 ndivyo vitakavyompa nguvu Ronaldo kutamba.
Kawa upande wa Makocha, Jurgen Klopp
atachuana na Makocha Magwiji wawili waliostaafu Mwaka 2013, Sir Alex
Ferguson wa Manchester United baada kuiongoza Klabu hiyo kwa Miaka 27 na
Jupp Heynckes alieifanya Bayern Munich itwae Trebo Mwaka Jana.
Kwa upande wa Kinamama, Wagombea wa Tuzo
ya Mchezaji Bora ni Nadine Angerer (Kipa toka Germany), Marta (Brazil),
ambae ameshaitwaa Tuzo hii mara 5 kati ya Mwaka 2006 na 2010, na Abby
Wambach (USA) ambae alitwaa ile ya Mwaka 2012.
Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa FIFA,
Jerome Valcke, amethibitisha kuwa katika Hafla hii ya Ballon d'Or
heshima maalum kwa Kiongozi wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, na
Lejendari wa Benfica na Portugal, Eusebio, waliofariki hivi karibuni,
zitatolewa.Eusebio alitwaa Ballon d'Or Mwaka 1965.
TUZO ZITAKAZOTOLEWA Jumatatu Januari 13:
FIFA Ballon d’Or
FIFA Mchezaji Bora Kinamama
FIFA Kocha Bora Timu za Wanaume
FIFA Kocha Bora Timu za Wanawake
FIFA Tuzo ya Rais
FIFA Tuzo ya Uchezaji wa Haki
FIFA Tuzo ya Puskas [Goli Bora]
FIFA/FIFPro Kombaini ya Dunia [Kikosi Bora cha Wachezaji 11]
No comments:
Post a Comment