Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, January 11, 2014

CHELSEA IKIWA UGENINI KC STADIUM, IMEIFUNGA HULL CITY MABAO 2-0 KWENYE LIGI KUU YA UINGEREZA

Chelsea wakiwa ugenini kucheza na Hull City huko kwenye Uwanja wa KC kipindi cha kwanza kilimalizika wakiwa nguvu sawa ya kutofungana ya 0-0. Chelsea wanaoshikilia nafasi ya tatu wakiwa na pointi 43 na Hull City wameshinda Mechi moja tu ya Ligi katika 7.Kipa wa Hull City McGregor akiokoa mkwaju wa frii kiki uliopigwa na mchezaji wa Chelsea
Kipindi cha pili dakika ya 56 Eden Hazard alifunga bao na kufanya blues kuwa 1-0 dhidi ya wenuyeji Hull City. Bao la pili la Chelsea limefungwa na Torres baada ya kuwachomoka mabeki upande wa kushoto na kuachia shuti kali lililompita mlinda mlango wa Hull City McGregor katika dakika za lala salama dakika ya 87.Eden Hazard akishangilia bao lake katika dakika ya 56 kipindi cha pili.


RATIBA/MATOKEO
Jumamosi Januari 11 

Hull City 0 v Chelsea 2
18:00 Cardiff City v West Ham
18:00 Everton v Norwich
18:00 Fulham v Sunderland
18:00 Southampton v West Brom
18:00 Tottenham v Crystal Palace
20:30 Manchester United v Swansea


Jumapili Januari 12
17:05 Newcastle V Man City
19:10 Stoke V Liverpool
Jumatatu Januari 13

23:00 Aston Villa V Arsenal

No comments:

Post a Comment