Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, December 13, 2013

THIERRY HENRY ATAMANI RIBERY ASHINDE TUZO YA BALLON d'Or

Nyota wa zamani wa klabu ya Arsenal na Barcelona Thierry Henry amesema angependelea kumuona winga wa Bayern Munich Frank Ribery akishinda tunzo ya Ballon d'Or this year.

Mshambuliaji huyo wa The New York Red Bulls ambaye amekuwa kifanya mazoezi na klaby take ya zamani ya Gunners wakati huu ambapo ligi ya nchini Marekani MLS ikiwa imekwisha ameeleza kuwa angependa nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa kushinda tuzo hiyo January 13 kwani mshambuliaji huyo si mbinafsi achezapo uwanjani akiwa na klabu yake lakini pia hata akiwa na timu yake ya taifa.

"Ribery ni mchezaji mkubwa na mwenye haiba ya kipekee anapokuwa uwanjani" Henry alikuwa akiongea na Sky Sports.

"anafikiria zaidi kutengeneza magoli kuliko kujitengenezea magoli.Ni aina ya mchezaji ambaye unapenda kucheza naye, napenda ashinde tuzo."

Ribery anakabiliana na ushindani kutoka kwa wakali wengine wa kufumania nyavu kutoka ligi ya Hispania Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.

No comments:

Post a Comment