SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), kwa kushirikiana na Benki
ya CRDB, wamejipanga kutoa elimu kwa mashabiki wa soka nchini juu ya mfumo mpya
matumizi ya tiketi za Kielektroniki zinazotarajiwa kuanza kutumika rasmi katika
raundi ya pili ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
CRDB ndio wazabuni walioshinda tenda ya kuuza aina hiyo ya
tiketi, ambazo mpaka sasa zimeanza kufanyawiwa majaribio ya mauzo katika mechi
ya Azam FC, dhidi ya RuvuShooting kwenye Uwanja wa Chamazi wiki iliyopita.
CRDB kwa kushirikiana na TFF, leo inatarajia kuendelea na mchakatop
wa majaribio ya mauzo ya tiketi, kupitia pambano la kirafiki maalum kwa ajili
baina ya Ashanti United dhidi ya Maafande wa JKT Ruvu.
Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alisema hayo leo kuwa,
wameamua kufanya hivyo kutokana na uelewa mdogo wa baadhi ya mashabiki wa soka,
uliodhihirika na mechi ya awali ya majaribio ya tiketi hizo.
Wambura alisema, elimu hiyo itatolewa kwa kina, kwani
wamegundua watu hawajui nini maana ya tiketi hizo kwani katika mchezo uliopita
walipata wakati mgumu juu ya suala hilo.
“Mchezo uliopita dhidi ya Azam FC na Ruvu Shooting, TFF na
CRDB tulipata wakati mgumu mara baada ya mashabiki kuja na pesa zao uwanjani
wakijua tiketi hizo zinapatikana pale moja kwa moja - wakati sio hivyo,”
alisema Wambura.
Aliongeza kuwa, TFF inaangalia uwezekano wa kuwapa semina
waandishi wa habri ili waweze kufikisha ujumbe kwa umma juu ya matumizi sahihi
ya mfumo huo wa tiketi za kielektroni.
No comments:
Post a Comment