KATIBU wa Chama cha Waamuzi Tanzania (FRAT) Charles Ndagala
amewapongeza waamuzi kwa uwezo wao mzuri waliouonesha katika kuchezesha
mashindano mbalimbali.
Ndagala aliyasema hayo wakati akifanya mahojiano maalum na
gazeti hili na kusema waamuzi wakiendelea na uwezo walionesha katika mwaka huu
ule usemi wa kuwa waamuzi ndio wanadidimiza maendeleo ya soka nchini utafutika
kabisa.
“Nawapongeza waamuzi wote waliopata nafasi ya kuchezesha
michezo yeyote nchini kuanzia ligi daraja la nne hadi Ligi Kuu Tanzania Bara
kwani wameonesha uwezo mkubwa na pia nawaomba waendelee hivyo ili ile dhana ya
waamuzi kuwa chanzo cha mchezo wa soka kutosonga mbele ifutike’, alisema
Ndagala.
Pia Ndagala ameupongeza uongozi mpya wa TFF chini ya Rais
Jamal Malinzi kwani amekuwa karibu nao pale anapohitaji ufafanuzi wa
kitaalamu kuhusu sheria 17 za soka
aliwafuata.
Katika kuhakikisha wanaboresha chama cha waamuzi FRAT
imeongeza mikoa miwili mipya katika wanachama wake ambayo ni mkoa wa Geita na
Katavi na kuitaka mikoa ya Njombe, Manyara na Simiyu kuhakikisha inaanzisha
darasa la waamuzi ili wapate wanachama wake.
Aidha Ndagala amesema kuwa Kmati ya Utendaji ya chama hicho
iliyokaa Desemba 15, mwaka huu imeazimia kuitisha mkutano Mkuu kwa ajili ya
kufanyia marekebisho katiba ya chama hicho ili kutoa wigo mpana wa kuwa na
wanachama kulingana na mahitaji ya sasa.
“Katiba ya FRAT kwa sasa inasema ili uwe mwanachama
unatakiwa uwe na miaka 23 jambo ambalo linakinzana na wakati tuliopo kwani
mashindano ya umri wa kuanzia miaka 12 inaanzishwa hivyo ili kuwapa fursa
waamuzi vijana kuwepo katika chama tutakirekebisha kipengele hicho na tumeamua
kufanya hivyo kwani TFF imetukabidhi waamuzi wa Twalipo na kwenye mikoa kuna
idadi kubwa ya waamuzi vijana”, alisema Ndagala
Pia Ndagala amewataka viongozi wa mikoa kuendelea na program
ya mazoezi ya kila mwisho wa wiki kwani inasaidia kuinua kiwango cha uamuzi
katika kuchezesha kutokana na uzoefu wanaobadilishana na kuwakumbusha kulipia
ada za uanachama mapema.
No comments:
Post a Comment