Wakati
msimu wa sherehe za Krismass na mwaka mpya ukiwa unazidi kushika kasi
huku mameneja wa vilabu vya England (Premier League) wakikosa usingizi
kwa hofu ya nini kitatokea kesho huko Hispania Real Madrid
iliwakutanisha pamoja nyota wao wa vikosi vya timu za mpira wa miguu na
kikapu ambao waliokuwa katika mitindo mbalimbali ya kisasa.
Hakukuwa
na mavazi ya ajabu ajabu yaliyoonekana ambapo wachezaji walikuwa huru
kunywa na wakifurahia milo huku wachezaji wa vikosi vyote wa Real
Madrid wakikusanyika kwa pamoja wakisheherekea mchana wa jana.
Wazo
la kuzindua sherehe za Krismass na mwaka mpya kwa mtindo wa chakula cha
mchana hapo jana Jumatatu linaonekana ni jambo la kawaida kwa
Waingereza ambapo Cristiano Ronaldo, Sergio Ramos
na Gareth Bale walijumuika na wenzao wenye uzoefu ambao si wazoefu sana
na mambo hayo ndani ya Bernabeu.
Cristiano Ronaldo (kulia) akiwa na mcheza kikapu nyota wa Real Madrid Marcus Slaughter wakiwa wamezungukwa na glasi za vinywaji
Gareth Bale (kulia) akitaniana na Mbrazil Marcelo
Rais Florentino Perez (katikati) akizungumza na wachezaji Marcelo na Gareth Bale
Nyota wa Los Blancos waliuungana na wachezaji klabu hiyo wa mchezo kikapu ikiwa ni pamoja na Marcus Slaughter na Dontaye Draper.
Kituko
ni pale Balozi wa klabu hiyo Zinedine Zidane alionekana mdogo
alipojipima urefu na wachezaji wa kikapu Salah Mejri na Ioannis
Bourousis ambao timu yao ya kikapu msimu uliopita walifika fainali ya
ligi ya mabingwa ya kikapu wakifungwa katika fainali na Olympiakos.
Zinedine Zidane (katikati) akionekana
mdogo kwa urefu ukilinganisha na wachezaji kikapu wa Real Madrid Salah
Mejri (kushoto) na Ioannis Bourousis
President Florentino Perez
(katikati), meneja Carlo Ancelotti (kushoto) na kocha wa timu ya kikapu ya Real Madrid Pablo Laso
President Florentino Perez akiongea na Raphael Varane (kushoto) na Alvaro Arbeloa (kulia)
Wachezaji
wa timu zote mbili za Real Madrid za kikapu na mpira wa miguu wakiwa
wamehudhuria sherehe za uzinduzi wa msimu wa krismas kwa timu yao ambazo
zilifanyika jana Jumatatu Estadio
Santiago Bernabeu
No comments:
Post a Comment