Wanachama wa Pan African wametakiwa kufuata ngazi husika pale wanapoona viongozi wa klabu yao wanakwenda kinyume na Katiba yao.
Kamati
ya Sheria na Hadhi za Wachezaji imetoa mwongozo huo kwa wanachama wa
Pan African baada ya kumwandikia barua Katibu Mkuu wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kulalamikia uongozi wao wakati wao si
wanachama wa TFF.
Wanachama
hao wanalalamikia uongozi wa klabu yao kwa kuitisha mkutano wa uchaguzi
kabla ya ule wa kawaida ambao unatakiwa kufanyika mara moja kwa mwaka.
Kamati
ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF imelazimika kutoa mwongozo huo
kwa vile wanachama hao katika malalamiko yao wamekigusa Chama cha Mpira
wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) ambacho ni mwanachama wa TFF.
Pan
African ni mwanachama wa Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Ilala
(IDFA) ambao ndiyo wanachama wa DRFA. Hivyo, TFF imemtaka mwanachama
wake DRFA kupitia IDFA kufuatilia tatizo hilo na kulipatia ufumbuzi.
MKUTANO WA WAANDISHI JB BELMONTE
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeitisha Mkutano na Waandishi wa
Habari utakaofanyika Desemba 31, 2013 saa 6 kamili mchana.
Mkutano huo utafanyika kwenye hoteli ya JB Belmonte iliyoko Jengo la NSSF Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment