Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, December 26, 2013

MANCHESTER CITY YAIFUNGA LIVERPOOL 2-1 KUSHIKA NAFASI YA PILI EPL

Liverpool ndio walioanza kufunga bao dakika ya 24 kupitia mchezaji wake Philippe Coutinho huku Manchester City wakisawazishiwa bao hilo na baki wao Vincent Kompany katika dakika ya 31 kipindi hicho hicho cha kwanza.Dakika za nyongeza dakika ya 45+1 kipindi cha kwanza City waliongeza bao kupitia mchezaji Álvaro Negredo na kupumzika City wakiwa juu ya bao moja. kipindi cha pili pamoja na kwamba kilikuwa ni nipige nikupige hakuna timu iliyoongeza bao. Timu zote hakuna iliyoziona nyavu kipindi cha pili. Ushindi huo wa mabao 2-1 unawapandisha City nafasi ya Pili kwenye msimamo wakiwa na pointi 38 Chini ya Gunners wenye pointi 39 ikiwa ni gepu la alama moja baada ya kuishindilia West Ham United bao 3-1 leo jioni. Timu inayoshika nafasi ya tatu ni Chelsea ya nne ni Liverpool kisha Everton.

Chezea City wewe: Kompany (kati) akishangilia baada ya kusawazisha bao hilo kipindi cha kwanza

Philippe Coutinho akiendesha mpira baada ya  kuachiwa na Raheem Sterling nakisha kuwapa bao Liverpool
Suarez akikimbizwa na Lescott pamoja na Yaya Toure

Chupuchupuu: Raheem Sterling aliachia mpira na mpira huo ukagonga posti ya goli kwa juu

Luis Suarez juu kwa juu na Joleon Lescott

City captain Vincent Kompany akidhihirisha kwamba yeye ni beki hapa!!

Negredo akiwawasha Majogoo bao la pili

Kipa Mignolet  hakuona ndani chuti la  Negredo.
VIKOSI:
Man City: Hart 7, Zabaleta 6, Kompany 7, Lescott 7, Kolarov 5, Y Toure 6, Fernandinho 7, Navas 8, Silva 7 (Garcia, 86), Nasri 6 (Milner 71, 6), Negredo 8 (Dzeko 76).
Subs not used: Pantilimon, Clichy, Boyata, Nastasic.
Goals: Kompany 30, Negredo 45
Booked: Zabaleta 80
Liverpool: Mignolet 6, Johnson 6, Sakho 7, Skrtel 6, Cissokho 5; Lucas 6 (Aspas, 81), Sterling 7, Henderson 7, Allen 6, Coutinho 6 (Moses, 67), Suarez 7.
Subs not used: Jones, K Toure, Agger, Alberto, Smith.
Goal: Coutinho 23.
Booked: Johnson, Moses, Suarez..
Man of the match: Jesus Navas.
Referee: Lee Mason 7.
Attendance: 47,351.

No comments:

Post a Comment