Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, December 20, 2013

KOCHA WA TIMU YA CARDIFF CITY MAJI YA SHINGO, ATAKIWA KUJIUZULU AU KIBARUA KUOTA MBAWA, JUMAMOSI YUPO UGENINI ANFIELD

Facing the axe: Cardiff boss Malky Mackay has been sent an ultimatum by Vincent Tan MENEJA wa Cardiff Malky Mackay yupo hatarini kuondoka Klabuni hapo baada ya kupewa tishio na Mmiliki wake Vincent Tan kwamba ajiuzulu mwenyewe ama atafukuzwa kazi.
Inadaiwa kuwa Vincent Tan, Raia wa Malaysia, alituma Barua pepe ikimtaka Malky Mackay, Miaka 41, ajiuzulu ama afukuzwe kazi.
Hali tete imeikumba Cardiff City tangu Mwezi Oktoba wakati Tan alipomtimua Mkuu wa Usakaji Vipaji na Usajili Wachezaji, Iain Moody, ambae alikuwa na uzoefu mkubwa na kumweka Kijana mdogo wa Miaka 23 kwenye nafasi hiyo. 

Hali ilizidi kuchafuka Klabuni hapo wakati Mtendaji Mkuu wake, Simon Lim, alipotoa Taarifa Siku ya Jumatatu kwamba Tan amekasirishwa sana na matakwa ya Malky Mackay ya kutaka Wachezaji wengine Mwezi Januari wakati mwanzoni mwa Msimu alitumia Pauni Milioni 50 kununua Wachezaji.
Lim aliongeza kuwa Mackay hatapewa hata Senti moja kuongeza Wachezaji hiyo Januari.
Licha ya kusakamwa, Mackay, ambae Mkataba wake unamalizika Mwaka 2016, amegoma kujiuzulu na anaendelea na kazi yake na leo anatarajiwa kuongea na Wanahabari katika Mahojiano ya kawaida kabla ya Mechi yao ya Jumamosi ambayo watasafiri kwenda Anfield kucheza na Liverpool.

Nae Brendan Rodgers, Meneja wa Liverpool, ambae ni Rafiki wa karibu wa Mackay, amemshambulia Vincent Tan kwa kumdhalilisha Rafiki yake na kumwambia Raia huyo wa Malaysia ‘hajui lolote kuhusu Soka!’

In the frame? Ole Gunnar Solskjaer has been touted with a move to the Premier League from Molde
Ole Gunnar Solskjaer wenda akapewa timu kama mambo yatazidi kwenda kombo kwa kocha Malky Mackay

Hadi sasa kwenye Ligi Kuu England, baada ya Mechi 16, Cardiff City wapo Nafasi ya 15 wakiwa Pointi 4 juu ya zile Timu 3 za mkiani ambalo ndio eneo la kushushwa Daraja.

MSIMAMO CARDIFF CITY ILIPO KWA SASA! 
MECHI ZIJAZO KWA CARDIFF CITY:
Saturday: Liverpool v Cardiff...........(12.45pm)
Boxing Day: Cardiff v Southampton....... (3pm)
Dec 28: Cardiff v Sunderland.............(5.30pm)
Jan 1: Arsenal v Cardiff..........................(3pm)
Jan 4: Newcastle v Cardiff......................(3pm)
(FA Cup 3rd round)
Jan 11: Cardiff v West Ham....................(3pm)

No comments:

Post a Comment