Polisi wanachunguza tukio ambapo kiungo wa timu ya taifa ya soka ya
Ghana Kevin - Prince BOATENG alishambuliwa mnamo Siku Kuu ya Krismasi
baada ya kuzuka ugomvi katika eneo la Kaarst nchini Ujerumani
Polisi karibu na mji wa Düsseldorf wamethibitisha tukio hilo wakisema
Boateng mwenye umri wa miaka 26 alishambuliwa akiwa barabarani na mtu
ambaye hakutambulika. Kiungo huyo anayechezea klabu ya Schalke 04
alipata majeraha madogo tu.
Gazeti la michezo la Bild liliripoti kuwa Boateng alimtembelea mtoto
wake wa kiume, nyumbani kwa mkewe wa zamani, mnamo Siku ya Krismasi,
wakati alipopigwa na mtu mmoja ambaye hakutambulika na akaanguka.
Boateng alizaliwa mjini Berlim na akaichezea Ujerumani katika kila
kiwango, lakini anaichezea timu ya taifa ya Ghana ambao wamepangwa na
Ujerumani, Ureno na Marekani katika Kundi G la dimba la Kombe la Dunia
nchini Brazil mwaka wa 2014.
No comments:
Post a Comment