Paris Saint-Germain ina mpango wa kuvunja rekodi ya dunia ya usajili wa pauni milioni £210 kwa ajili ya Lionel Messi.
Taarifa
kutoka jijini Paris zinasema mabingwa hao wa ligi kuu ya nchini
Ufaransa 'Liegue 1' wanataka kuvunja kibubu kwa ajili ya msambuliaji
huyo mwenye umri wa miaka 26 kwa kuvunja mkataba wake na Barcelona.
Kwasasa
mshambuliaji huyo anaonekana ni kama ni mwenye sintofahamu ndani ya Nou
Camp kufuatia maoni ya mkurugenzi Javier Faus juu uboreshaji wa mkataba
wake.
Lionel Messi akiwa katika picha ya pamoja na mkewe Antonella Roccuzzo mjini Rosario
Messi bado yuko katika mkataba wa
pauni milioni £13.5 ambapo utamuweka katika klabu yake mpaka 2018 ambapo
Faus alikaririwa akisema Messi huenda akapewa 'package bora' kufuatia
ongezeko la pauni milioni £15 kwa mwaka kwa mshambuliaji wa timu pinzani
Cristiano Ronaldo.
Messi aliyekuwa na hasira alikaririwa akisema
'Faus ni mtu ambaye hajui lolote kuhusu soka na kwamba anataka kuiendesha Barelona kibiashara kitu ambacho sio sawa'
Endapo PSG watafanikiwa katika mpango
huo itakuwa ni ada zaidi ya mara mbili ya rekodi ya uhamisho ya
wachezaji duniani ambayo inashikiliwa na Gareth Bale ya pauni milioni
£86.
No comments:
Post a Comment