
Jack Wilshere wa Arsenal akijaribu kumkaba mchezaji wa Tiote wa Newcastle leo kwenye ligi kuu England
Olivier
Giroud ameifungia bao la kichwa timu yake Arsenal katika Dakika ya 65
leo limeifanya Arsenal iifunge Newcastle huko St James Park Bao 1-0 na
kutwaa tena uongozi wa Ligi Kuu England wakiwa Pointi 1 mbele ya
Manchester City.
Ingawa Arsenal walifungua nafasi kadhaa za kufunga
lakini ni Newcastle waliokosa Bao za wazi wakati Shuti la Moussa Sissoko
lilipookolewa na Kichwa cha Mathieu Debuchy kupiga posti.
Goli hilo la Arsenal lilipatikana baada ya Frikiki ya Theo Walcott kuunganishwa na Giroud.
Ushindi huu umewafanya Arsenal wawe kileleni mwa Ligi Kuu England Siku ya Mwaka mpya kwa mara ya kwanza tangu Msimu wa 2007/08.

Tiote leo alikuwa nuksi kwenye ukabaji

Bosi
wa Timu ya Arsenal Arsene Wenger akimnyooshea refa mkono kwa kile
alichokiona kuwa si sawa uwanjani leo, Gunners wakiwa ugenini Kwa
Newcastle.

Majanga!!

Tiote kwenye patashika kuutwaa mpira wa kichwa

Hapa baada ya kufanyiwa ndivyo sivyo!!

Olivier akiruka juu baada ya kuukosa Mpira

Nipishe nipite!!
No comments:
Post a Comment