Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, November 5, 2013

FA YAMBANA SASCHA RIETHER WA FULHAM KWA RAFU YA MAKUSUDI KWA KINDA ADNAN JANUZAJ BAADA YA MWAMUZI LEE PROBERT KUTOMWADHIBU

Riether atakubali adhabu hiyo au atakataa?Mchezaji beki wa Fulham Sascha Riether amefunguliwa Mashitaka ya Fujo Uwanjani kwa kumkanyaga kwa makusudi Adnan Januzaj wakati Manchester United inaichapa Fulham Bao 3-1 Uwanjani Craven Cottage hapo Jumamosi kwenye Mechi ya Ligi Kuu England.
Refa wa Mechi hiyo, Lee Probert, hakuliona tukio hilo lakini Jopo la Watu watatu la FA wanaoshughulikia matukio ya aina hiyo walipitia Video na kuamua kumfungulia Mashitaka Mchezaji huyo wa Fulham.
Riether amepewa hadi Jumanne Novemba 5 Saa 3 Usiku, Bongo Taimu, ili kujibu Mashitaka hayo ambayo huenda yakampa Kifungo cha Mechi ya 3 na kuendelea au Faini au vyote kwa pamoja.
Akiongelea kuhusu Mechi yao ya UEFA CHAMPIONZ LIGI ya Jumanne Usiku huko Spain na Real Sociedad, Meneja wa Man United, David Moyes, awe analindwa Uwanjani kwani amekuwa akiwindwa.

Moyes alisema: “Inaonekana ni makusudi. Nadhani anahitaji kulindwa zaidi kupita anavyopewa.”Kocha wa Manchester United David Moyes.

No comments:

Post a Comment