Ghana
wamejiweka pazuri kuliona lango la Brazil baada ya kuwafunga Egypt bao
6-1 usiku leo kwenye mpambano mkali wa kuwania Tiketi ya kwenda Brazil
Mwakani kucheza Fainali za Kombe
la Dunia kwenye Uwanja wa BABA YARA STADIUM huko Kumasi Nchini Ghana,
Ghana ndio walianza kupata bao dakika ya 4 bao la Gyan na akifunga bao
lake la 2 kipindi cha pili dakika ya 54, Bao la pili wamejifunga wenyewe
baada ya mchezaji kuwakaanga mabeki wa Egypt na kujichanganya dakika ya
22 kupitia mchezaji wao Wael Gomaa kumfunga kipa wake, Ghana waliongeza
nguvu dakika ya mwishoni mwa kipindi cha kwanza dakika ya 44 A. Waris
akafunga bao safi. Kipindi
cha kwanza kimemalizika Ghana wakiwa juu ya mabao 3-1 dhidi ya Egypt.
Dakika ya 73 kipindi cha pili Sulley Ali Muntari akawaongezea bao Ghana
kwa mkwaju wa Penati. Dakika za lala salama kwenye dakika ya 89mchezaji
C. Atsu
akatupia bao la mwisho la 6. Na mpira kumalizika kwa 6-1. Bao la pekee
la Egypt limefungwa kwa mkwaju wa penati dakika ya 41 kipindi cha kwanza
kupitia mchezaji wao Mohamed Abo Trika. Jumanne Novemba tarehe 19
watarudiana Egypt kwao na Ghana saa 1 za Usiku, je? Egypt watalipiza
kisasi!!!
Mechi za Kwanza:
Jumanne Oktoba 15
19:00 Ghana v Egypt
USO KWA USO:
-Egypt Ushindi 9, Ghana Ushindi 4, Sare 5 na leo Ghana wameifunga 6-1 Egypt, Ghana wakitimiza ushindi wa 5.
AFRIKA
Raundi ya Mwisho ya Mtoano
MATOKEO:
Mechi za Kwanza:
Jumanne Oktoba 15
Ghana 6 v 1 Egypt
Jumamosi Oktoba 12
Burkina Faso 3 Algeria 2
Ivory Coast 3 Senegal 1
Jumapili Oktoba 13
Ethiopia 1 Nigeria 2
Tunisia 0 Cameroon 0
RATIBA:
Marudiano:
Jumamosi Novemba 16
18:00 Nigeria v Ethiopia
22:00 Senegal v Ivory Coast
Jumapili Novemba 17
17:30 Cameroon v Tunisia
Jumanne Novemba 19
19:00 Egypt v Ghana
21:15 Algeria v Burkina Faso
No comments:
Post a Comment