MABINGWA wa ligi kuu soka Tanzania Bara
Yanga Sc hii leo wameondoka na pointi tatu baada ya kuitandika Rhino ya
tabora mabao 3-0 katika mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara uliopigwa
kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Aidha mahasimu wao wa jadi Simba Sc ambao leo walikuwa ugenini mjini Tanga wakikwaana na wenyeji Coastal Union wamejikuta wakibanwa mbavu na kulazimishwa sare tasa.
Yanga ambayo ushindi wa leo umepoza machungu ya sare ya mabao 3-3 waliyoipata dhidi ya mahasimu wao Simba jumapili iliyopita, iliutawala mchezo huo ambapo ilipata ushindi wake kupitia kwa Hamis Kiiza aliyefunga mawili na Frank Domayo aliyefunga bao moja.
Mbali na mechi hizo, hii leo kulikuwa na mtanange mwingine uliozikutanisha Tanzania Prisons ya Mbeya dhidi ya Kagera Sugar ambapo Kagera nayo imetoshana nguvu kwa bao 1-1.
Simba yalazimisha suluhu Tanga na Coastal Union
Coastal Union wamelazimishwa suluhu katika uwanja wa nyumbani wa Mkwakwani walipokutana na wekundu wa Msimbazi Simba.
Katika kipindi cha kwanza Simba walionekana kuelemewa kiasi golikipa wa timu hiyo Mganda Abel Dhaira alishindwa kustahamili mikiki ya Mganda mwenzake wa Coastal union, Yayo Kato ambaye alikuwa hampi nafasi. Hivyo Dhaira akasalimu amri dakika chache kabla ya kipindi cha kwanz akuisha na nafasi yake ikachukuliwa na golikipa namba mbili wa Simba Abuu Hashim.
Mpaka dakiak 45 za awali zinakwisha hakuna timu iliyoona lango la mwenzake lakini kwa namna Wagosi walivyokuwa wakishambulia kwa kasi walifurahi sana mwamuzi alipopuliza kipyenga kuashiria ni mapumziko.
Kipindi cha pili Simba walianza kwa kasi ambayo iliwatisha mashabiki wa Coastal, lakini haikudumu kwa muda mrefu mambo yakaanza kuwabadilikia.
Baada ya kuona hakuna mtu wa kutumbukiza mipira katikati, kocha wa Wagosi Joseph Lazaro, ambaye amechukua nafasi ya Hemed Moroco aliyeachia ngazi alimuingiza Uhuru Suleiman na kumtoa Danny Lyanga, halafu akamtoa Keneth Masumbuko na kumuingiza Pius Kasambale.
Mbali ya mabadiliko hayo bado uhaba wa mabao uliendelea kuiandama Coastal Union huku Simba wakiomba mchezo uishe kutokana na kuelemewa kila idara.
Katika hatua nyingine wana kidedea waliokuwa wakipiga ngoma walishikwa na bumbuwazi wasijue cha kufanya kutokana na ugumu wa mechi.
Simba ambao wametoka suluhu ya 3-3 na Simba Jumapili iliyopita hawakufurahishwa na suluhu ya leo mbali ya kuja na uongozi wote kuanzia Mwenyekiti Aden Range, Makamu Mwenyekiti Mzee Kinesi na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Hanspope.
Kutokana na suluhu hiyo Wagosi wa Kaya wamevuna point 12, huku wakiendelea kushikilia nafasi ya 9 katika msimamo. Baada ya hapo watakabiliwa na mechi dhidi ya Mtibwa Sugar na Mgambo JKT zote zitachezwa Mkwakwani. Baada ya hapo watatoka nje kucheza na JKT Ruvu katika uwanja wa Chamazi jijini Dar es Salaam.
RATIBA:
Jumatatu Oktoba 28
Coastal Union vs Mtibwa Sugar
Oljoro JKT vs Ashanti United
Ruvu Shooting vs Kagera Sugar
Simba vs Azam
Jumanne Oktoba 29
Tanzania Prisons vs Mbeya City
Yanga vs Mgambo Shooting
Rhino Rangers vs JKT Ruvu
Alhamisi Oktoba 31
Simba vs Kagera Sugar
Ijumaa Novemba 1

MSIMAMO: ULIVYO KWA SASA.
NA | TIMU | P | W | D | L | GD | GF | PTS |
1 | Simba SC | 10 | 5 | 5 | 0 | 12 | 20 | 20 |
2 | Azam FC | 10 | 5 | 5 | 0 | 9 | 15 | 20 |
3 | Mbeya City | 10 | 5 | 5 | 0 | 6 | 13 |
20
|
4 | Yanga SC | 10 | 5 | 4 | 1 | 10 | 21 | 19 |
5 | Mtibwa Sugar | 10 | 4 | 4 | 2 | 4 | 16 | 16 |
6 | Ruvu Shooting | 10 | 4 | 3 | 3 | 3 | 12 | 15 |
7 | Kagera Sugar | 10 | 4 | 3 | 3 | 3 | 11 | 15 |
8 | JKT Ruvu | 10 | 4 | 0 | 6 | -2 | 9 | 12 |
9 | Coastal Union | 10 | 2 | 6 | 2 | 1 | 7 | 12 |
10 | Ashanti UTD | 10 | 2 | 3 | 5 | -9 | 10 | 9 |
11 | Prisons FC | 10 | 1 | 5 | 4 | -7 | 6 | 8 |
12 | Rhino Rangers | 10 | 1 | 4 | 5 | -7 | 8 | 7 |
13 | JKT Oljoro | 10 | 1 | 3 | 6 | -8 | 8 | 6 |
14 | Mgambo Shooting | 10 | 1 | 2 | 7 | -15 | 3 | 5 |
RATIBA:
Jumatatu Oktoba 28
Coastal Union vs Mtibwa Sugar
Oljoro JKT vs Ashanti United
Ruvu Shooting vs Kagera Sugar
Simba vs Azam
Jumanne Oktoba 29
Tanzania Prisons vs Mbeya City
Yanga vs Mgambo Shooting
Rhino Rangers vs JKT Ruvu
Alhamisi Oktoba 31
Simba vs Kagera Sugar
Ijumaa Novemba 1
JKT Ruvu vs Yanga
Jumamosi Novemba 2
Mgambo Shooting vs Coastal Union
Tanzania Prisons vs Oljoro JKT
Azam vs Ruvu Shooting
Mtibwa Sugar vs Rhino Rangers
Mbeya City vs Ashanti United
Jumatano Novemba 6
JKT Ruvu vs Coastal Union
Ashanti United vs Simba
Kagera Sugar vs Mgambo Shooting
Rhino Rangers vs Tanzania Prisons
Ruvu Shooting vs Mtibwa Sugar
Alhamisi Novemba 7
Azam vs Mbeya City
No comments:
Post a Comment