Na Mwandishi
Wetu.Kigoma
KAMPUNI ya
Tanzania Breweries Limited (TBL) imetoa kiasi cha shilingi milioni 7.2
katika shindano la mbio la wasooza mitumbwi kwa kipindi cha mwaka 2013
lililofanyika katika Ziwa Tanganyika Mkoani Kigoma.
Akikabidhi
fedha hizo kwa washindi wa shindano hilo, katibu tawala wa Wilaya ya Kigoma bw.
Joshua Elisha amewataka washindi hao kutumia vyema fedha walizozipata katika
kuinua uchumi wa maisha yao.
Amesema kuwa
kupitia michezo hiyo inayofanyika kila mwaka mkoani Kigoma ni njia mojawapo ya
kuwaweka watu pamoja kwa kushirikiana kuboresha maslahi yao pamoja na
biashara zao kwa kununua vifaa vya kisasa vya kuvulia mazao ya samaki na
dagaa.
“Fedha hii
isiwe sababu ya kuanza malumbano ya kikundi ni lazima kama kikundi kufanya uwekezaji
kwa kuboresha zana za kuvulia na kuacha tabia ya kutumia zana ambazo
haziruhusiwi kisheria kufanyia shughuli za uvuvi, halafu faida itakayo patikana
ndio kila mmoja anufaike kupitia uwekezaji uliofanyika awali” amesema bw.
Elisha.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti mwenyekiti wa chama cha mbio za mitumbwi Taifa bw.
Richard Mgabho na mwenyekiti wa Mkoa wa Kigoma bw. Huseni Hatibu wamesema kuwa
mashindano hayo ni endelevu na washindi wa mkoa wa Kigoma watashiriki
shindano la Kikanda jijini Mwanza ambapo waliwataka washindi hao kufanya
mazoezi kwa bidii na kuacha tabia ya kutumia mbinu za kishirikina.
Wamesema
kuwa katika shindano la ukanda wa ziwa mikoa itakayo shiriki ni pamoja na
Kagera, Msoma, Kigoma pamoja na jiji la Mwanza ambapo donge nono litatolewa kwa
mshindi atakaye shinda katika shindano la kanda ya ziwa.
Aidha
washindi hao kwa upande wa wanaume ni kikundi cha Makila kimeibuka mshindi wa
kwanza na kujinyakulia shilingi laki tisa, mshindi wa pili beach Boy Katonga
laki saba, watatu Katonga A kapata laki tano na mshindi wan nne Katonga
Beach kapata laki nne, huku mshindi wa tano hadi kumi wamepata shilingi
laki mbili na nusu kati ya vikundi 23 vilivyo shiriki ambapo mshindi wa kwanza
hadi wa tatu watashiriki shindano la kikanda jijini Mwanza hivi karibuni.
Kwa upande
wa wanawake mshindi wa kwanza ni kikundi cha Mwamgongo kapata laki saba, wa
pili Remba kapata laki sita, watatu Best Gerezi kapata laki nne na wan ne
Tanganyika kapata laki tatu huku mshindi wa tato hadi kumi wamepata kali mbili
kila kikundi kati ya vikundi 14 vilivyo shiriki ambapo msindi wa kwanza na
wapili nao watashiriki shindano la kikanda.
Hata hivyo
mwakilishi wa kampuni hiyo Mkoa wa Kigoma bw Kasile Kasile amesema kuwa lengo
la kampuni kuweka mashindano hayo ni kutaka kurudisha fadhila kwa wateja
wao ikiwa ni pamoja na kuinua uchumi na kuboresha maisha ya wavuvi nchini
sambamba na kushiriki katika miradi ya kimaendeleo
No comments:
Post a Comment