Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, October 20, 2013

MWANANYAMALA MABINGWA WA KOMBE LA MEYA WA KINONDONI, WAKABIDHIWA BAJAJI, FEDHA TASLIMU MILIONI 2 NA JEZI

Naibu waziri wa mawasiliano, sayansi na teknolojia, Mhe. Januari Makamba (kushoto) akiteta jambo na meya wa manispaa ya kinondoni, Yusuph Mwenda. Naibu waziri wa mawasiliano, sayansi na teknolojia, Mhe. Januari Makamba (kushoto) akizungumza na wakazi wa manispaa ya kionondoni. kushoto kwake ni meya wa manispaa hiyo Yusuph Mwenda na naibu meya wa manispaa hiyo Songoro Mnyonge. Mshambuliaji wa Mwananyamala Rashidi Kidebe (kushoto0 akiwania mpira na beki wa kawe kombaini Emmanuel Nengu. Naibu waziri wa mawasiliano, sayansi na teknolojia, Januari Makamba (kushoto) akikabidhi jezi kwa nahodha wa timu ya kawe Issa Kitasa ambao ni washindi wa pili wa michuano hiyo.
Naibu waziri wa mawasiliano, sayansi na teknolojia, Januari Makamba (katikati) akikabidhi kombe kwa nahodha wa timu ya kawe Issa Kitasa ambao ni washindi wa pili wa michuano hiyo. kulia ni meya wa manispaa hiyo, yusuph mwenda. Naibu waziri wa mawasiliano, sayansi na teknolojia, Januari Makamba (wa pili kulia) akikabidhi kombe kwa nahodha wa timu ya Mwananyamala, Ramadhani kipanya baada ya timu yake kuibuka mabingwa wa michuano ya kombe la meya wa kinondoni. kulia ni meya wa manispaa hiyo, yusuf mwenda.

Na Fadhili Akida
Mwananyamala mabingwa wa kombe la meya wa kionondoni dhidi ya kawe kombaini, wakabidhiwa bajaji, fedha tasilimu milioni 2 na jezi katika fainali iliyofanyika uwanja wa magunia, msasani dar es salaam.

Timu ya soka ya Mwananyamala jana waliibuka mabingwa wa kombe la meya wa kinondoni na kukabidhiwa zawadi za bajaji, fedha tasilimu milioni 2 na jezi. akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi hizo naibu waziri wa mawasiliano, sayansi na teknolojia, januari makamba aliwaasa vijana hao kutumia vema zawadi hizo ikiwemo fedha na bajaj kwa kusaidia maendeleo yao ikiwemo kuboresha maisha yao. makamba alimsifu meya wa manispaa hiyo yusuph mwenda kwa kuandaa mashindano hayo ambayo yanasaidia kuwaleta vijana pamoja na kudumisha mshikamano na amani baina yao. kwa upande wake meya wa manispaa hiyo, yusuf mwenda alisema huo ni mwanzo tu wa kampeni yake ya kuweka safi manispaa yake ambapo kupitia michezo anawahamasisha wakazi wa manispaa hiyo kuweka safi mazingira yanayowazunguka.

No comments:

Post a Comment