Aliyekuwa meneja wa klabu ya
Manchester United ya Uingereza Sir Alex Ferguson amesema David Beckham
alilazimika kuondoka katika klabu hiyo kutokana na tabia yake ya
kujiona ni mkubwa kuliko meneja wake.
Katika kitabu kipya kuhusu historia ya maisha
yake Ferguson amesema enzi za uongozi wake walitofautiana na Beckham
kutokana na kumkosoa kuhusiana na kiwango chake katika matokeo ya ligi
ya FA 2003.
Mchezaji huyo alionekana kuwa na msimamo unaoonyesha kujiona mkubwa na kutokubali maelekezo .
Furguson amesema kuwa tabia ya Beckham
ilionekana kubadilika tangia alipomuoa mwanamuziki maarufu wa miondoko
ya pop Victoria kutoka kundi la Spice Girls
"David ni mchezaji pekee ambaye nilimuwezesha
kumuweka katika mazingira ya umaarufu wa soka kidunia, lakini
sikufurahishwa na maisha ya umaarufu wake na hasa kujiona yeye ni bora
zaidi' alisema Ferguson.
Ferguson amesema haijalishi ni Alex Furguson ama
Pete the plumber, lakini mamlaka ni mamlaka tu, hangeweza kuwa na
mchezaji ambaye haheshimu mamlaka,nadhan kama ni kuondoka ni bora
alivyoondoka tu.
Beckham aliyeshinda mara sita katika ligi ya
Premier ya uingereza,vikombe viwili vya FA na moja katika Champions
League akiwa na klabu hiyo baadaye aliuzwa kwa Real Madrid kwa dola
million 25 katika msimu wa joto 2003,kabla ya kwenda nchini Marekani
kuchezea klabu ya LA Galaxy.
Sir Alex Ferguson yeye amestaafu mwezi May mwaka
huu umeneja katika klabu hiyo ya Manchester huku akiwa ni miongoni mwa
mameneja walifikia mafanikio makubwa katika historia ya kuiongoza timu
hiyo.
No comments:
Post a Comment