MABAO
matatu aliyofunga mshambuliaji wa kimataifa Uholanzi Robin van Persie
katika ushindi wa mabao 8-1 dhidi ya Hungary wa mechi za kufuzu michuano
ya Kombe la Dunia umemfanya kuwa mshambuliaji aliyefunga mabao mengi
zaidi katika nchi yake. Van Persie alifikisha mabao 41 katika mechi 80
alizocheza katika timu ya taifa na kuizidi rekodi iliyowekwa na Patrik
Kluivert katika mechi hiyo iliyopigwa jana usiku. an
Persie ambaye anacheza katika klabu ya Manchester United alifunga bao
la kuongoza kwa timu yake katika dakika ya 15 kabla ya kuifikia rekodi
hiyo ya mabao ya taifa kwa kufunga bao lingine kabla ya mapumziko. Nyota
huyo aliongeza bao lingine katika dakika 52 na kufanya idadi ya mabao
aliyoifungia timu ya taifa kufikia 41 na kumpita Kluivert aliyekuwa
akishikilia rekodi hiyo kwa kufunga mabao 40.
No comments:
Post a Comment