LONDON,
England
LIGI Kuu ya England kwa sasa ni kama
imekomaa, ambapo kwa miaka kadhaa yamekuwa yakishuhudiwa mabao yenye kiwango
cha hali ya juu kutoka kwa wachezaji ambao hawawezi kusahaulika.
Wakati msimu huu zikiwa
zimeshafanyika mechi takribani saba, jambo la kujiuliza ni kwanini msimu huu
ligi hiyo inaonekana kuwa kali kuliko miaka yote.
1.
Matumizi
ya fedha
Tangu miaka ya nyuma Ligi Kuu ya
England haijawahi kuwa na matumizi makubwa ya fedha wakati wa usajili, lakini
mwaka huu klabu za Uingereza msimu huu zimevunja rekodi kwa kutumia pauni
milioni 630 katika dirisha la usajili.
Kiasi hicho cha fedha kimevunja
rekodi ya pauni milioni 500, ambazo timu hizo zilizitumia wakati wa usajili wa
wa mwaka 2008.
Fungu hilo la fedha linadaiwa
linatokana na fedha ambazo klabu zote zililipokea msimu uliopita, baada ya viongozi
wa ligi hiyo kuingia mikataba na vituo vya televisheni ili kuwekeza kiasi
kikubwa cha fedha kwenye michuano ya ligi hiyo.
2.
Mbio za
ubingwa
Inaelezwa kuwa kwa miaka mingi ya
nyuma, haijawahi kutokea idadi kubwa ya timu zinazofukuzia ubingwa wa ligi hiyo
na badala yake zilikuwa ni timu nne tu zilizokuwa zikijitokeza kufukuzia
ubingwa huo.
Hata hivyo msimu huu imeshuhudiwa msururu
mrefu wa timu zikiwania kutwaa taji hilo.
Katika mbio za sasa timu za Chelsea, Spurs, Man United, Arsenal, Liverpool
na Man City, tayari zimeshaanza kuonesha mchuano mkali huku Arsenal ikiwa imekaa kileleni kwa pointi mbili
zaidi dhidi ya wapinzani wao.
3.
Vipaji
vipya
Wakati zikiwa zimeshatumia fedha
kupindukia, kipindi hiki pia ni cha klabu za Uingereza kuongeza vipaji vipya.
Baadhi ya mifano ya vipaji vilivyorudishwa
msimu huu ni kama Juan Mata, Christian Benteke na Michu.
Hata hivyo msimu huu imeshuhudiwa
vikitua vipaji vingine vipya vyenye wachezaji wenye uwezo mkubwa kama vile Christian
Eriksen, Mesut Ozil, Wilfred Bony, Maarten Stekelenburg, Willian na Ricky Van
Wolfswinkel.
Mbali na vipaji vya wageni, pia kuna
nyota wachache raia wa England kama vile
Andros Townsend na Ross Barkley ambao wameshaanza kuonesha uwezo wake kwenye michuano
ya Ligi Kuu.
4.
Timu
hazitabiriki
Suala la timu kutotabirika ni kati
ya vitu vinavyoongeza chachu katika ligi hiyo msimu huu na matokeo yake
yamekuwa yakiwashangaza wengi.
Miongoni mwa matokeo yaliyowashtua
wengi, ni kipigo cha mabao 3-2 ilichokutana nacho Manchester City kutoka kwa
Aston Villa.
Mbali na matokeo hayo pia
ilishuhudiwa mabingwa watetezi, Manchester United wakichapwa mabao 2-1 na West Brom huku ikishuhudiwa Chelsea chini ya Jose Mourinho ikilala kwa bao 1-0 dhidi ya Everton.
Pia Aston Villa imeshuhudiwa
ikilamba pointi zote tatu kutoka kwa Arsenal na huku Southampton ikiiduwaza Liverpool kwa kuichapa
bao 1-0.
Matokeo hayo yanaifanya Ligi Kuu
hiyo kuonekana kuwa ngumu kuliko mtu yeyote anavyoidhania.
5.
Msaada
Huku ikiwa imesheheni matangazo ya
bidhaa za biashara, michezo ya video, Ligi Kuu haijawahi kupata msaada mkubwa
kwa ajili ya klabu zote kama ilivyo sasa.
Kwa sasa Ligi Kuu inapatikana kila pembe ya duniani,
hivyo kila mtu anaweza kuangalia ligi
hiyo bora duniani.
No comments:
Post a Comment