Shrikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa za
kifo cha mjumbe wa Bodi ya klabu ya Ashanti United, Jimmy Mhango
kilichotokea jana (Oktoba 21 mwaka huu).
Msiba
huo ni mkubwa kwa wadau wa mpira wa miguu kwani Mhango aliutumikia
mpira wa miguu kwa muda mrefu, tangu akiwa mchezaji, kocha na baadaye
kiongozi.
Kabla
ya kuingia kwenye Bodi ya Ashanti United, enzi za uchezaji wake
alichezea timu za Mapinduzi ya Dodoma, Ushirika ya Moshi na Pan African
ya Dar es Salaam. Pia aliwahi kuwa Kocha Mkuu wa Ashanti United.
TFF
inatoa pole kwa familia ya marehemu Mhango, klabu ya Ashanti United na
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), na kuwataka kuwa
na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
Maziko
yamefanyika leo mchana katika makaburi ya Abeid (Mchikichini) Dar es
Salaam. Mungu aiweke roho ya marehemu Mhango mahali pema peponi. Amina
No comments:
Post a Comment