Wenger:
Sikutaka kumsajili Flamini
LONDON, England
KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger ametobao siri kwamba, hakuwa
na mpango wa kumrudisha kikosini kwake kiungo Mathieu Flamini, lakini kiwango
kilichoonyeshwa na Mfaransa huyo kwenye mazoezi kilimfanya abadili uamuzi na
kumsajili. Flamini aliondoka Arsenal mwaka 2008 na kujiunga AC Milan, ambako
alichemka na wakati wa kiangazi alikuja Emirates kwa ajili ya kufanya mazoezi
na kujiweka fiti tu, lakini Wenger akakunwa na kiwango chake na kuamua kumpa
mkataba.
@@@@@
Mignolet:
Moses, Sakho watatisha Anfield
LIVERPOOL, England
KIPA wa Liverpool, Simon Mignolet, anaamini mastaa wapya wa
klabu hiyo, Victor Moses na Mamadou Sakho watakuja kufanya makubwa sana siku za
usoni, Moses aliyetua Liver kwa mkopo akitokea Chelsea na Sakho amesajiliwa kwa
pauni milioni 15 kutoka PSG, Jumatatu walikuwa kwenye kikosi cha Liverpool kilichopata
sare ya mabao 2-2 na Swansea na wote walionyesha kiwango kikubwa huku, Moses
akifunga bao moja jambo ambalo lilimsababisha kipa hiyo wa Kibelgiji kuamiani
kwamba wawili hao watakuja kufanya makubwa sana Anfield.
@@@
Pato:
Madaktari wa AC Milan walinizingua
RIO
DE JANEIRO, Brazil
STRAIKA wa Corinthians, Alexandre Pato ameishukia klabu yake
ya zamani ya AC Milan na kudai kwamba madaktari wa klabu hiyo ndiyo sababu ya
yeye kusugua benchi kwa muda mrefu alipokuwa San Siro kutokana na kusumbuliwa
majeruhi. Pato anaamini kwamba, matatizo ya misuli yaliyokuwa yakimsumbua
yalisababishwa na madaktari ambao walimruhusu kurudi mapema uwanjani wakati
akiwa bado hajapona vizuri.
@@@@
Bale:
Ronaldo, Zidane watanifanya niwe bora
MADRID,
Hispania
GARETH Bale anaamini atakuwa bora zaidi Real Madrid,
kutokana na kufanya mazoezi na wachezaji wenye viwango bora katika klabu hiyo,
Bale alimmwagia sifa Cristiano Ronaldo na kudai kwamba anatarajia kujifunza
mengi kutoka kwa Mreno huyo, huku pia akidai kwamba uwepo wa Zinedine Zidane
kwenye benchi la ufundi la timu hiyo, kutamsaidia kufikia kiwango cha juu zaidi
duniani na kutimiza malengo yake.
No comments:
Post a Comment