DAKIKA za mwisho kabla ya
dirisha la usajili kufungwa, Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, alivunja rekodi
ya klabu hiyo kwa kutoa pauni milioni 42 ili kupata saini ya kiungo mchezeshaji
mwenye kiwango bora duniani, Mesut Ozil.
Nyota huyo wa Ujerumani
anayekipiga Real Madrid,
alifanya mazungumzo na Wenger asubuhi ya siku ya mwisho ya dirisha la usajili
na kukubali kumwaga wino kwenye klabu hiyo ya Emirates. Je, Wenger ataendelea
kusajili wachezaji wenye viwango? Ni wachezaji gani watakuwa chaguo lake wakati
wa dirisha dogo la usajili Januari mwakani? Wafuatao ni baadhi ya wachezaji
ambao Wenger, alikuwa akiwafukuzia au anaweza kuwasaka majira ya baridi
5.
Micah Richards, Manchester
City
Beki wa Ufaransa, Bacary Sagna,
akiwa hadi sasa hajasaini mkataba mpya kwenye klabu hiyo ya Emirates, tayari
Wenger anaonekana amepata mtu atakayeziba nafasi yake, mchezaji huyo ni beki wa
kulia mwenye umri wa miaka 26 kutoka Man City, Micah Richars. Richards anaweza
akawa muhimu kwenye safu ya ulinzi ya Arsenal, kwa uchezaji wake wa kutumia
nguvu na kuwa na akili za kuweza kuiongoza safu ya ulinzi ataweza kuwa msaada
mkubwa kwa Gunners.
4.
Ashley Williams, Swansea
City
Arsenal walifanya mazungumzo na nahodha huyo
wa Wales wakati wa msimu wa kiangazi, lakini hawakumaliza mipango ya uhamisho. Ashley Williams, aliweka wazi kuwa anataka kucheza
klabu ambayo inashiriki Ligi ya Mabingwa. Ubora wake na uwezo wa kuzoeana na
mabeki wenzake, kunamfanya awe chaguo sahihi kuwa beki wa kati wa Gunners, hata
katika nafasi ya beki wa kulia.
3.
Michu, Swansea City
Mchezaji mwingine kutoka katika klabu ya Swansea City,
Michu, ambaye pia alifanya mazungumzo na klabu hiyo ya Kaskazini mwa London. Ni mshambuliaji
aliyefanya vizuri msimu uliopita na kupachika mabao 22 katika mechi 43, thamani
yake ni pauni milioni 25 kwa mujibu wa klabu yake. Wenger anafikiri kuwa nyota
huyo wa Hispania anaweza kuwa msaada katika safu ya ushambulia ya Gunners.
2.
Edwin Dzeko, Manchester
City
Nyota huyo wa Bosnia, alikuwa kwenye mpango wa
klabu hiyo ya Arsenal wakati wa harakati za usajili majira ya kiangazi. Kocha
wa Man City, Manuel Pellegrini, yuko tayari
kumuachia, Dzeko aondoke na kumfanya Wenger aingie kichaa cha kumfukuzia.
Kutokana na kuwasili kwa wachezaji kama
Jovetic na Negredo, ambaye tayari ameanza kuonyesha shughuli katika kupachika
mabao ndani ya Etihad, kunamfanya Dzeko akose nafasi na kutoa upenyo kwa Wenger
kukamilisha mipango yake ya kumnasa mshambuliaji huyo.
1.
Luis Suarez, Liverpool
Bila shaka Luis Suarez, ndiye aliyekuwa chaguo
la kwanza la Wenger katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi. Nyota huyo
wa Uruguay,
mwenye umri wa miaka 26, anaonekana kuwa mchezaji sahihi katika safu ya
ushambuliaji ya Arsenal. Akichezeshwa pamoja na Ozil wanaweza kufanya mambo ya
kushangaza England
hata na Ulaya. Lakini ni kitu gani kocha wa Gunners atafanya, kuweza kuwasajili
wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu na kuifanya klabu hiyo ya kaskazini mwa London kuwa tishio.
No comments:
Post a Comment