MADRID,
Hispania
IMEFAHAMIKA kuwa kiungo wa Real Madrid, Sami Khedira,
anataka kumfuata Mjerumani mwenzake, Mesut Ozil aliyetua Arsenal katika siku ya
mwisho ya dirisha la usajili la kiangazi. Uwepo wa Asier Illarramendi na kuaminika
kwa Luka Modric, kunamfanya Khedira kukosa namba kwenye kikosi cha kwanza cha Madrid. Arsene Wenger
bado anataka kuongeza kiungo mkabaji kwenye timu yake licha ya kuwepo kwa
Mathieu Flamini.
@@@@@@
Moyes
kukomaa na Benteke Januari
MANCHESTER, England
KOCHA wa Manchester United, David Moyes ameendelea na
mchakato wake wa kutaka kumsajili straika wa Aston Villa, Christian Benteke
wakati wa Januari, licha ya Benteke kuongeza mkataba na Villa wakati wa
kiangazi, lakini Moyes anaonekana kutokukata tamaa kuwania saini ya staa huyo
wa Ubelgiji, ambaye msimu uliopita alikuwa moto wa kuotea mbali kutokana na
kufunga mabao 23, na msimu huu tayari ameshatupia nyavuni mabao matano.
@@@@@@
Everton,
Newcastle
vitani kwa Doumba
LONDON, England
EVERTON na Newcastle United, zimeingia kwenye
vita ya kumuwania straika wa CSKA Moscow, Muivory Coast Seydou Doumba,
inasemekana Newcastle imekuwa ikiwania saini yake kwa zaidi ya mwaka mmoja
sasa, Alan Pardew anaamini atamnasa jamaa huyo Januari, lakini anatarajia
kupata wakati mgumu kutoka kwa Roberto Martinez wa Everton ambaye na yeye kwa
sasa anasaka straika wa kuongeza nguvu kwenye safu yake ya ushambuliaji
No comments:
Post a Comment