Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, September 14, 2013

ULIMWENGU AIPAISHA TP MAZEMBE NA KUFUZU NUSU FAINALI



MSHAMBULIAJI  wa Tanzania Thomas Ulimwengu leo waliiwezesha klabu yake ya TP Mazembe kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la shirikisho baada ya kuifungia mabao mawili kati ya manne iliyoshinda .

Ulimwengu ambaye ni mchezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania alikuwa nyota wa mchezo huo kati ya Tp Mazembe na Entente Sportive Setiff ya Algeria ambao  walishinda mabao 4-2 mchezo uliocyhezwa huko Lubumbashi nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Thomas Ulimwengu alifunga mabao mawili kwenye mchezo huo huku moja likiwa la kichwa lilitokana na mpira wa krosi ya Mbwana Samatta.

Mabao mengine la TP Mazembe yalifungwa na mkongwe na nyota wa timu hiyo Tressor Mabi Mputu moja likiwa kwa njia ya penati huku Setif wakipata mabao yao kupitia kwa Mohamed Zeiti na Kaled Gourmi.

Matokeo haya yanaipeleka TP Mazembe kufuzu kucheza hatua ya nusu fainali ya kombe la shirikisho wakiwa wamejikusanyia pointi 10 baada ya michezo mitano huku wakiwa wamebakiwa na mchezo mmoja kabla ya hatua ya makundi kumalizika.

No comments:

Post a Comment