Mechi
hiyo itachezwa Septemba 7 mwaka huu jijini Banjul, Gambia ambapo Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premiem Lager itaondoka kesho
(Septemba 4 mwaka huu) saa 11 alfajiri kwa ndege ya Kenya Airways
kupitia Dakar, Senegal.
Kim
amesema wanataka kushinda ugenini, kwani licha ya kuwa wameshatolewa
lakini ushindi utawaongezea pointi kwa ajili ya viwango (rankings) vya
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na pia kuepuka kuanzia
ngazi ya awali ya mechi za mchujo za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON)
kwa fainali za 2015.
“Tunacheza
mechi hii tukiwa katika mazingira magumu, kwani wengi wa wachezaji wa
kikosi cha kwanza ni majeruhi. Sijawahi kukutana na hali hii tangu
nilipoanza kuifundisha Taifa Stars, lakini tumejipanga kuhakikisha
tunafanya vizuri,” amesema Kim.
Amesema
kwa mipango ya timu yake mechi hiyo ni muhimu tofauti na wengi
wanavyofikiria, na uamuzi wake wa kumwita beki Henry Joseph amezingatia
mambo mengi ya kiufundi ikiwemo nafasi anayocheza na uzoefu wa mchezaji
aliyekuwa akicheza nchini Norway katika klabu ya Kongsvinger IL.
Wachezaji
majeruhi katika kikosi hicho ni Shomari Kapombe, Kelvin Yondani, Aggrey
Morris, Salum Abubakar, Athuman Idd na John Bocco.
Vilevile
wachezaji Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu hawatakuwemo kwenye safari
baada ya klabu yao ya TP Mazembe kutuma taarifa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) leo mchana ikidai ni wagonjwa.
Wachezaji
wanaoondoka kwenda Banjul ni Juma Kaseja, Mwadini Ali, Ali Mustafa,
Amri Kiemba, David Luhende, David Mwantika, Erasto Nyoni, Frank Domayo,
Haruni Chanongo, Henry Joseph, Jonas Mkude, Juma Liuzio, Khamis Mcha,
Mrisho Ngasa, Nadir Haroub, Said Dilunga, Simon Msuva na Vincent
Barnabas.
No comments:
Post a Comment