SIMBA SC imepunguzwa kasi
na Mbeya City
baada ya kulazimishwa sare ya 2-2 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
Bara Uwanja wa Taiafa, Dar es Salaam.
Pamoja na matokeo hayo, Simba SC bado inaongoza Ligi Kuu kwa kufikisha pointi 11 baada ya kucheza mechi tano, wakati Mbeya City inafikisha pointi saba baada ya mechi tano pia.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na Abdallah Kambuzi wa Shinyanga, Charles Mbilinyi na Juma Mwita wa Mwanza, hadi mapumziko, tayari Simba SC walikuwa mbele kwa mabao 2-1
Simba SC inayofundishwa na Abdallah Athumani Seif ‘King
Kibaden’, ilipata mabao yake yote kupitia kwa Amisi Tambwe aliyefunga katika
dakika za 29 na 33.
Mbeya City, inayofundishwa na Juma Mwambusi, bao la kipindi cha kwanza lilifungwa na Paul Nonga dakika ya 37, wakati la kusawazisha lilifungwa na Richard Peter dakika ya 69.
Tambwe alifunga bao lake la kwanza akiunganisha krosi ya Chanongo, wakati la pili ilikuwa pasi ya Betram Mombeki.
Kikosi cha Simba SC
kilikuwa; Abbel Dhaira, William Lucian ‘Gallas’, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Kaze
Gilbert, Joseph Owino, Jonas Mkude, Twaha Ibrahim, Amri Kiemba, Betram Mombeki,
Amisi Tambwe na Haroun Chanongo.
Mbeya City; David Buruhan, John Kabanda, Hassan Mwasapili, Deogratius Julius, Antony Matogolo, Yohana Morris, Mwagane Yeya, Steven Mazanda, Paul Nonga, Deus Kaseke na Yussuf Willson.
Katika mechi nyingine, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga wenyeji Mgambo Shooting Stars walitoka sare ya 1-1 na Rhino Rangers ya Tabora.
Prisons ilitoka 1-1 na Mtibwa Sugar Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine
mjini Mbeya, wakati Kagera Sugar ilishinda 3-0 dhidi ya Ashanti United ya Dar es Salaam Uwanja wa Kaitaba.
Ligi hiyo itakamilisha mzunguko wake wa tano leo kwa mechi tatu moja ndiyo hiyo ya Azam na Yanga Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam huku JKT Ruvu ikikwaruzana na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Azam Complex.
Ruvu Shooting inayokamata nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi itakuwa mgeni wa Coastal Union katika mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
No comments:
Post a Comment