TIMU ya JKT Mlale ya Songea jana iliifunga Kurugenzi ya
Njombe bao 1-0 kwenye mchezo wa ligi daraja la kwanza uliochezwa Uwanja wa
Majimaji, Ruvuma.
Mchezo huo ambao ulikuwa wa ushindani ulishuhudia timu zote
zikienda mapumziko bila kufungana.
Kipindi cha pili JKT Mlale walipoingia walipata bao kupitia
kwa Ally Mohamed kunako dakika ya 54 baada ya kuachia shuti kali lililokwenda
moja kwa moja wavuni.
Kwenye Uwanja wa Nang’wanda Sijaona Mtwara Villa Scuad
walitoka sare ya 0-0 na wenyeji Ndanda.
Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza wenyeji Pamba walitoshana nguvu
na Polisi Dodoma kwa kufungana mabao 3-3.
Timu ya Africa lyon iliifunga Tesema bao 1-0 kwenye mchezo
uliochezwa Uwanja wa Karume jijini Dar
es Salaam.
Mjini Shinyanga wenyeji Stand United waliwachezesha kwata
maafande wa Polisi Tabora kwa kuwafunga bao 1-0 mchezo uliochezwa Uwanja wa
Kambarage.
No comments:
Post a Comment