LONDON, England
KWA
lugha rahisi, unaweza kusema kuwa siku ya leo mtoto hatumwi sokoni.
Usemii
huu utadhihirika leo wakati miamba ya soka nchini England, Manchester United na
Liverpool, itakaposhuka uwanjani kuumana, zikiwania pointi tatu muhimu kwenye
michuano ya Ligi Kuu ya England.
Mbali
na timu hizo, pia kuna mtihani mwingine kwa Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger,
ambaye kibarua chake kipo shakani, baada ya kulazimishwa kusajili wachezaji
wapya, lakini yeye akaamua kuweka njiti masikioni.
Mechi
hizo zote ni muhimu kwa kila timu kutokana na kuwa ndizo zitakazotoa mwelekeo
wa kila timu katika michuano ya mwaka
huu. Kwa mujibu wa historia ya timu hizo, Liverpool FC na –Manchester United FC, ni timu
zenye ushindani mkubwa katika soka la England na pia timu hizo mbili ni kati ya
timu zenye mafanikio makubwa kwenye michuano hiyo, zikiwa zimefanikiwa kutwaa
mataji 121, 59 yakiwa ni ya Liverpool na 62 ya Manchester United.
Ukiachilia
mbali ushindani viwanjani, timu zote mbili ni kati ya timu zinazoingiza kipato
kikubwa na pia ni timu ambazo zina mashabiki wengi kwenye ulimwengu wa soka.
Viwango
vya timu: Man United itakwenda kukikabili kikosi hicho cha Merseyside, ikiwa
na kumbukumbu ya Jumatatu ilipotoka sare na mahasimu wao, Chelsea, katika
mtanange uliopigwa kwenye Uwanja wa Old Trafford, mechi ambayo ilikuwa mtihani
wa kwanza mkubwa kwenye utawala wa David Moyes.
Matokeo
hayo yalikuja ikiwa ni baada ya timu hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi
ya Swansea City na mabingwa hao wa msimu uliopita watakuwa wakitaka kurudia
rekodi hiyo watakaposhuka kwenye dimba hilo la Anfield, licha ya jambo hilo kuonekana
halitakuwa rahisi kwa timu kama Liverpool, ambayo imeshajikusanyia pointi nzuri
kutoka kwenye mechi dhidi ya Stoke City na
Aston Villa, zilizoifanya kuwa moja kati ya timu mbili zilizokwishajiwekea
rekodi kwenye Ligi Kuu hiyo ya Barclays.
*Ndani
na Nje: Katika mtanange huo, Wayne Rooney anaweza kurejea kwenye nafasi
yake ya kuanza kikosi cha kwanza, baada ya Jumatatu kuonesha kiwango kizuri na
huku Ashley Young naye akitarajia kuwamo
kikosini.
Kwa
upande wao, Rafael na Javier Hernandez wao
bado hawataonekana uwanjani kutokana na kuwa bado ni majeruhi na huku Nani naye
akionekana kuwa huenda akaikosa mechi hiyo.
Kwa
upande wake Liverpool, Martin Skrtel, anaweza kuwemo uwanjani, lakini kikosi
hicho cha Brendan Rodgers kitakuwa hakina wachezaj kama vile Kolo Toure, Joe Allen na Aly Cissokho, ambao
waliumia wakati wa mechi ya Kombe la Ligi
iliyopigwa Jumanne wii hii dhidi ya timu ya Notts County.
Kivutio katika mchezo huo kitakuwa ni mfungaji bora wa mwaka jana, Robin Van Persie, ambaye mabao yake yaliisaidia klabu hiyo ya Old Trafford kutwaa ubingwa msimu uliopita, huku Liverpool ikimkosa nyota wake, Luis Suares ambaye amefungiwa.
Msimu huu tayari Van Persie ndiye aliyefunga bao la kwanza kabla ya kuunganisha pande alilotengewa na Nemanja Vidic, kabla ya timu hizo kenda mapumziko wakati, Daniel Sturridge naye akitarajia kuonesha uwezo wake.
*Nyota wa mechi: Baada ya kujiunga na Liverpool akitokea Chelsea mapema Januari mwaka huu, Daniel Sturridge alijidhihirisha kuwa mmoja wa silaha za maangamizi baada ya kuifungia mabao 12 dakika za mwisho msimu uliopita.
Na katika mwendelezo huo nyota huyo aliyekulia kwenye timu ya watoto ya Manchester City msimu huu, ameshafunga mabao manne katika mechi tatu alizokwishacheza msimu huu.
Kutokana na hali hiyo, inaelezwa kuwa mabeki wa Manchester United ni lazima wahakikishe wanamchunga vilivyo mshambuliaji huyo.
*Wachezaji wanavyosema
Kwa upande wa wawachezaji, beki wa Manchester United, Rio Ferdinand, anasema kuwa anaihofia safu ya ushambuliaji ya Liverpool, inayoundwa na wachezaji Danny Sturrrige na Philippe Countino.
Nadhani ni wachezaji wazuri waliosajiliwa mwishoni mwa msimu uliopita. Daniel Sturridge anaonekana kuwa ni mchezaji hatari na Philippe Countino ni mchezaji mzuri,” alisema beki huyo.
*Makocha: Kwa upande wa makocha, Brendan Rodgers ana uhakika vijana wake hawataathirika na dakika 120 walizocheza Jumanne wakati Man Uted itakapowatembelea leo.
“Tumewapa muda wa kutosha wa kupumzika wachezaji,” aliiambia tovuti ya Liverpool. “Haya ndiyo mawazo ya kwamba nitawatumia baadhi ya wachezaji wakongwe kutokana na kwamba kutakuwepo na ushindani, lakini na kwa kuwachezesha wachezaji vijana kutawasaidia kuwajengea uwezo wa kucheza kwenye mechi zenye ushindani,” alisema kocha huyo, mara baada ya mechi hiyo ya Kombe la Ligi.
Alisema hadi kufikia mtanange wa leo tayari wachezaji wake watakuwa wamepumzika na hivyo atakuwa amejiandaa vilivyo kuwakabili wapinzani wake.
Wakati Rodgers akijitapa hivyo, kwa upande wa Man United, kocha wa zamani wa Everton kwa uzoefu wake wa miaka 11 akiwa na timu hiyo, David Moyes, anazifahamu vilivyo mechi zinazozikutanisha timu hizo na kwamba raia huyo wa Scotland ataingia uwanjani akiwa hana hofu kubwa kuhusu mechi hiyo.
*Waamuzi: Andre Marriner, ndiye atakayekuwa katikati ya dimba hilo la Anfield.
Mara ya mwisho mashabiki wa Manchester United kumuona ilikuwa ni Machi mwaka huu, wakati timu yao ilipoibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Reading katika mechi za Kombe la FA.
Kivutio kwa mwamuzi huyo ni pale msimu uliopita alipowazawadia kadi nyekundu wachezaji watano.
*Mechi tano za mwisho zilizozikutanisha timu hizo
15 Oktoba 2011
|
Liverpool
|
1-
1
|
Manchester United
|
Anfield, Ligi Kuu
|
|
28 Januari 2012
|
Liverpool
|
2–1
|
Manchester United
|
Anfield Kombe la
FA
|
|
11 Februari 2012
|
Manchester United
|
2–1
|
Liverpool
|
Old Trafford, Ligi Kuu
|
|
23 Septemba 2012
|
Liverpool
|
1–2
|
Manchester United
|
Anfield,Ligi Kuu
|
|
13 Januari 2013
|
Manchester United
|
2–1
|
Liverpool Old ,
Trafford
|
Ligi Kuu
|
*Arsenal v Tottenham Hotspur:
Wakati roho za mashabiki wa Liverpool na Man United zikiwapaa, mvutano mwingine utakuwa ni kati ya Tottenhm na Arsenal ambao utapigwa kwenye uwanja wa Emirates muda wa saa 10 kwa saa za England.
*Vikosi, Arsenal ambayo huenda ikatumia mfumo
wa , 4-2-3-1 huenda ikawatumia wachezaji kama
Szczesny; Sagna, Koscielny, Mertesacker, Gibbs; Ramsey, Wilshere;
Walcott, Rosicky, Cazorla; Giroud.
Wakati Arteta, Diaby, Oxlade-Chamberlain, Podolski na Vermaelen hawatakuwamo uwanjani kutokana na kuwa majeruhi.
Tottenhma, 4-2-3-1): Lloris; Walker, Dawson,
Vertonghen, Rose; Capoue, Paulinho; Townsend, Dembélé, Chadli; Soldado.
Wakati Bale, Lennon, Assou-Ekotto, Adebayor hawatacheza kutokana na hali zao kiafya.
*Mwamuzi wa pambano hilo atakuwa ni Michael Oliver.
*Habari za timu.
Inaelezwa kuwa licha ya macho yote kuwa uwanjani kwa muda wa dakika zote 90 za mchezo huo, lakini akili zote zitakuwa ni kuhusu usajili wa Arsenal, baada ya timu hiyo kushindwa kutoa fedha kusajili mchezaji yoyote.
Hali hiyo inadaiwa kuwa italifanya benchi la ufundi la Arsenal kukaa tumbo joto kutokana na kwamba wanakutana na Tottenham ambayo ina kikosi kigumu.
*Historia ya hivi karibuni
Nyumbani 21-10,Ugenini 12-5,Sare 13-5.
*Mechi tano za mwisho kukutana Emirates.
Katika mechi hizo tano za mwisho zilizoikutanisha miamba hiyo zilizalisha mabao 30.
No comments:
Post a Comment