Mkurugenzi
wa Kampuni ya Lino Agency, Hashimu Lundenga akifafanua jambo wakati
akitangaza viingilio vya shindano la Redd’s Miss Tanzania jijini Dar es
Salaam jana, ambapo VIP, itakuwa Sh. 100,000 na sehemu ya kawaida sh.
50,000. Shindano hilo litafanyika Septemba 21 katika ukumbi wa Mlimani
City. Kushoto ni Meneja wa kinywaji cha Redd’s, Victoria Kimaro.
Meneja wa kinywaji cha Redd’s, Victoria Kimaro akitangaza wasanii watakaotumbuiza.
Na Mwandishi Wetu
WAKATI
zikiwa zimebaki siku tatu ili Redd’s Miss Tanzania ajulikane, viingilio
kwa ajili ya shindano hilo linalosubiriwa kwa hamu kubwa na Watanzania
wengi vimetangazwa.
Kiingilio
cha juu katika shindano hilo linalotarajiwa kufanyika keshokutwa
(Jumamosi) katika Ukumbi wa Mlimani City, uliopo Mwenge, Dar es Salaam
ni Sh 100,000 kwa viti maalumu, huku viti vya kawaida vikiwa Sh 50,000.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa kinywaji
cha Redd’s Original, Victoria Kimaro, ambao ndio wadhamini wakuu wa
Redd’s Miss Tanzania alisema, wanaamini viingilio hivyo ni vya kawaida
kutokana na ubora wa shindano lenyewe.
Victoria
alisema, burudani katika shindano hilo inatarajiwa kutolewa na msanii
mahiri kutoka Uganda, Mike Ross atakayeshirikiana na Judith Wambura
‘Lady Jaydee’ pamoja na kundi la Mama Afrika katika kukonga nyoyo za
mashabiki watakaojitokeza ukumbini hapo.
“Tunaamini
kabisa wasanii hawa watakonga nyoyo za mashabiki wa tasnia ya urembo
hapa nchini, hivyo napenda kutoa wito kwa mashabiki kujinunulia tiketi
mapema ili kuepuka usumbufu,” alisema Victoria.
Naye
Lady Jadee alisema, kwa kushirikiana na bendi yake ya Machozi
wamejipanga vizuri kuhakikisha wanatoa burudani ya nguvu kwa mashabiki
wote watakaohudhuria.
“Nawaomba
mashabiki wangu na wale urembo kujitokeza kwa wingi ili kufurahia
burudani nzuri toka kwangu na bendi yangu ya Machozi, pia wasanii
wenzangu waalikwa naamini watafanya vizuri siku hiyo,” alisema.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Lino International Agency, Hashimu Lundenga ambao ni
waratibu wa Redd’s Miss Tanzania alisema, tiketi za shindano hilo tayari
zimeshaanza kuuzwa katika vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Alitaja
maeneo ambayo yameteuliwa kuuza tiketi za Redd’s Miss Tanzania kwa
mwaka huu ni duka la Shear Illusion lililopo Mlimani City, City Sports
Lounge na Steers zilizopo Mtaa wa Samora, Faberk Fashion, Rose Garden
Pub na ofisi za Redd’s Miss Tanzania ambazo zote zipo eneo la Mikocheni.
“Kwa
mara nyingine tena napenda kuwashukuru wadhamini wetu wakuu kinywaji
cha Redd’s Original na wadhamini wenza ambao kwa kweli wamefanya kazi
kubwa sana kuhakikisha shindano la mwaka huu linakuwa zuri na lenye tija
kubwa.”
Lundenga
alifafanua kuwa, ili kuwapa fursa watu wengi zaidi tiketi
itakayonunuliwa katika vituo vilivyopangwa kabla ya shindano itakuwa ni
Sh 80,000 na kutakuwa na ofa kadhaa.
Taji la Redd’s Miss Tanzania kwa sasa linashikiliwa na Brigitte Alfred, aliyefanikiwa kulitwaa mwishoni mwa mwaka jana.
Shindano
la Redd’s Miss Tanzania linadhaminiwa na kinywaji cha Redd’s Original
kinachozalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), huku
wadhamini wenza wakiwa kinywaji cha Zanzi, hoteli ya Giragge, Star TV,
gazeti la Nipashe, Uchumi Supermarket na Marie Stopes.
No comments:
Post a Comment