Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, September 4, 2013

GARETH BALE vs CRISTIANO RONALDO UTAKUWA MUUNGANO HATARI ZAIDI


REAL Madrid wamekamilisha rasmi taratibu za kumsajili mshambuliaji wa Tottenham Hotspurs, Gareth Bale.
Kusajiliwa kwa mchezaji huyo kunamfanya aungane na straika bora kabisa wa Madrid, Cristiano Ronaldo, katika kusukuma mashambulizi ya timu hiyo.
Hali hiyo itaifanya timu hiyo kuwa na muungano hatari zaidi kwenye safu ya ushambuliaji, kutokana na wawili hao kuwa na rekodi zinazokaribiana.

GARETH BALE
Namba ya jezi: 11
Nafasi: Kiungo mshambuliaji
Umri: Miaka 24
Kuzaliwa: Julai 16, 1989
Alikozaliwa: Cardiff, Wales
Urefu: Futi 6 inchi 1 (1.83m)
Uzito: Kilo 74

****
CRISTIANO RONALDO
Namba ya jezi: 7
Nafasi: Mshambuliaji
Umri: Miaka 28
Kuzaliwa: Februari 5, 1985
Alikozaliwa: Madeira, Ureno
Urefu: Futi 6 inchi 1 (1.85m)
Uzito: Kilo 75

MSIMU ULIOPITA

MECHI WALIZOCHEZA
Ronaldo 30
Bale    34

MAGOLI
Ronaldo 34
Bale    21

MASHUTI GOLINI
Ronaldo 235
Bale    165

MASHUTI YALIYOLENGA
Ronaldo 105
Bale     73

PASI ZA MABAO
Ronaldo 10
Bale     4

RAFU WALIZOCHEZA
Ronaldo  27
Bale     24

RAFU WALIZOCHEZEWA
Ronaldo   81
Bale      47

KADI ZA NJANO
Ronaldo   9
Bale      6

KADI NYEKUNDU
Ronaldo  0
Bale     0

******
THAMANI ZAO
Bale
Bale alihamia Spurs kutoka Southampton mwaka 2007 kwa kitita cha Pauni milioni 5 tu, inasemekana anatua Madrid kwa Pauni milioni 78.

Ronaldo
Alitua Manchester United akitokea Sporting Lisbon ya Ureno kwa kitita cha Pauni milioni 12.5 mwaka 2003 na kisha akatua Madrid kwa Pauni milioni 80.
(Hii inamaanisha kuwa ungeweza kuwanunua akina Bale 16 kwa bei ya Ronaldo wakati ule)



Bale
Kwa kutazama nje, nyota huyo wa Tottenham Hotspur, anaonekana kwamba ataweza kufiti katika mfumo wa Real Madrid kama atakuwa mchezaji wa klabu hiyo.
Winga huyo wa Wales, aina ya soka lake linafanana na la Ronaldo kwa kiasi fulani, kwa maana ya kasi, nguvu na chenga za aina yake.
Alichukuliwa na Spurs kutoka katika klabu ya Southampton kwa kitita cha Pauni milioni 5 tu mwaka 2007. Kipindi hicho, mchezaji huyo ndani ya kikosi cha Spurs ameweza kupandisha kiwango chake cha soka na kuwa moja ya mastaa wanaotetemesha soko la usajili kwa kipindi hiki.
Kwa aina ya uchezaji wake wa sasa, akiwa chini ya kocha Andre Villas-Boas, Bale ameweza kuonyesha kwamba ni tishio kubwa anapocheza kama mshambuliaji wa kati.
Uwepo wake kwenye kikosi cha Spurs, ambacho safu yake ya ushambuliaji imekuwa ikibadilika, lakini kuwapo kwa mchezaji huyo kumeifanya timu hiyo ya Ligi Kuu England kuwa na makali ya aina yake.
Kama ilivyo kwa Ronaldo, Bale ni mchezaji wa muda mrefu, kwamba unaweza kuwekeza kupitia yeye na ukawa kwenye mipango kwa muda mrefu zaidi.
Uwezo wake wa umaliziaji ni wa aina yake na kuhesabiwa kuwa mmoja wa washambuliaji ulimwenguni, huku anamiliki pia kiwango kikubwa cha uchezeshaji, kitu ambacho kinaweza kumpa nafasi ya kucheza katika klabu yoyote. Je, atafiti kwenye mfumo wa Madrid?

Ronaldo
Ni straika wa aina yake, ambaye ni gumzo ulimwenguni.
Kumekuwa na imani kwamba Mreno huyo anatumia uvumi uliopo kwamba alitaka kurudi United ili kuifanya Real Madrid kutoa fedha nyingi kumbakiza, lakini ukweli halisi mchezaji huyo alifanikiwa kuishawishi Madrid ikamwongezea mkataba mnono.
Ronaldo si mchezaji tofauti sana na yule aliyehama United mwaka 2009, kwa sasa amezidi ubora wake zaidi. Kama Bale atapangwa naye, hakuna shaka kwamba ataendelea kutumika kama winga, ambayo ni nafasi yake ya asili.
Ni wazi kabisa kocha wa Madrid anaweza kufanya mabadiliko ya namba kwa ajili ya kukiweka sawa kikosi chake. Ronaldo atapewa nafasi pia ya kuzunguka uwanja mzima kutafuta mipira. Na kwenye hilo, Madrid haitaweza kutumia mfumo wa 4-2-3-1 kwa sababu jambo hilo litaacha nafasi kwenye kikosi, hasa kwa upande wa wachezaji wa pembeni.

No comments:

Post a Comment