Promota
wa Mpambano wa Ubingwa wa UBO Kaike Siraju katikati akiwanyoosha mikono
juu mabondia Ramadhani Shauri kushoto na Cosmasi Cheka watakaopigana Octoba 27 jijini Dar es salaam
|
MPAMBANO
WA mwingine wa masumbwi unatarajia kufanyika Oktoba 27 katika ukumbi
wa Friends Coner Manzese Dar es salaam litakalo wakutanisha mabondia
Ramadhani Shauri na Cosmas Cheka mpambano huo ulidhaminiwa na Hotel ya
Tanamera ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani
Akizungumza
mratibu wa mpambano huo Kaike Siraju amesema amepata sapoti katika
hotel hiyo ili aweze kuendeleza vipaji vya vijana unakumbuka mimi ndie
ninayeandaa mapambano makubwa nchini kama utakumbuka ila nilisimama
kidogo kwa ajili ya kutafakari na kurekebisha mambo yangu binafsi lakini
kwa sasa nimekuja kuinua mchezo huu kwa vijana chipkizi kwanza ndio
msingi wa ngumi duniani kote
Aliongeza
kwa kutaja mapambano ya utangulizi kuwa ni Mohamed Matumla anamenyana
na Sadiki Momba huku Amosi Mwamakula akizichapa na Hamisi Ajali na Juma
Fundi atazipiga na Shabani Kilumbelumbe
No comments:
Post a Comment