ARSENAL 3 v STOKE CITY 1
Arsenal wakicheza kwenye uwanja wao
Emirates leo jumapili ndio walianza kuifunga Stoke City dakika ya 5
kupitia mchezaji wao Ramsey baada ya Mesut Ozil kupiga frii kiki na
kuelekea upande wa pili mwa goli ambako kipa wa Stoke ameutema na
hatimaye Aaron kuumalizia mpira huo nyavuni. Dakika
ya 26 Stoke wakasawazisha kupitia mchezaji wao Geoff Cameron.
Kusawazisha bao hilo kukafanya Arsenal waongeze kasi ya kutafuta bao
jingine haraka na dakika ya 36 mchezaji Per Mertesacker akawafungia bao
jingine kwa kichwa na kufanya kipindi cha kwanza cha dakika 45 kuisha
Arsenal wakiwa mbele kwa mabao 2-1. Kipindi cha pili dakika ya 72 mchezaji Bacary Sagna akawaongezea bao la tatu kwa kichwa safi na kufanya bao 3-1 dhidi ya Stoke City.
Wachezaji
wa Arsenal wakifurahia baada ya mwenzao Ramsey kufunga bao dakika ya 5
Mesut Ozil akiachia frii kiki na kuelekea upande wa pili ambako kipa wa
Stoke ametema na hatimaye Aaron kuumalizia mpira huo nyavuni.Aaron akifurahia baada ya kutupia bao lake dakika ya 5Mtu kati hapa!Mesut Ozil akimtoka mchezaji wa Stoke City.
Per Mertesacker akipongezwa baada ya kufunga bao la kichwa dakika ya 36.Gnabry akimpiga chenga mchezaji wa Stoke Huth kipindi cha pili.Kocha wa Stoke City Stoke Mark Hughes hoi!!Kocha wa Gunners Mzee Wenger akilalamika hapa baada ya mchezaji wake kuumiaMesut Ozil akiendesha.Mesut Ozil akichonga frii kiki hapaHapa huna chako kaa pembeni!!Bacary Sagna na Charlie Adam wote chini!!Per Mertesacker ukafika muda akawaamusha mashabikiAaron Ramsey akichuana vikali na Geoff Cameron Jack Wilshere akibanwa na wachezaji wa StokeMesut Oezil hakushikika leo hiiBacary Sagna akifurahia baada ya kuzamisha bao la tatu na la mwisho hapa, bao alilofunga kwa kichwa.
VIKOSI:
Arsenal (4-3-2-1): Szczesny 6;
Sagna 7, Mertesacker 7, Koscielny 7, Gibbs 7; Flamini 8, Wilshere 6
(Monreal 73), Ramsey 7; Gnabry 5 (Ryo 73), Ozil 8 (Arteta 81); Giroud 6.
Subs not used: Vermaelen, Viviano, Bendtner, Jenkinson
Stoke (4-3-2-1): Begovic
5; Cameron 6, Shawcross 6, Huth 6, Pieters 5 (Palacios 67); Wilson 6,
N'Zonzi 6, Adam 6 (Ireland 59, 5); Walters 5, Arnautovic 6; Jones 6
(Pennant 75).
Subs not used: Whelan, Crouch, Etherington, Crouch, Sorensen
Referee: Mike Dean
Man of the match: Ozil
RATIBA/MATOKEO
Jumapili 22 Septemba
15:30 Arsenal 3 v 1 Stoke City
15:30 Crystal Palace 0 v 2 Swansea City
18:00 Cardiff 0 v 1 Tottenham Hotspur
18:00 Manchester City 4 v 1 Manchester United
No comments:
Post a Comment