Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imetoa tangazo la uchaguzi wa Kamati ya mpya ya Utendaji ambao utafanyika Oktoba 20 mwaka huu. Pia Kamati hiyo imetoa tangazo za uchaguzi wa Bodi ya Ligi Kuu ya Tanzania (TPL Board) ambao utafanyika Oktoba 18 mwaka huu.
Akitangaza mchakato huo wa uchaguzi leo (Agosti 14 mwaka huu) jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Hamidu Mbwezeleni amesema nafasi zitakazogombewa kwa upande wa TFF ni Rais, Makamu wa Rais na wajumbe 13 wa Kamati ya Utendaji wakiwakilisha kanda mbalimbali.
Fomu kwa wagombea zitatolewa kuanzia Agosti 16 mwaka huu kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 10 kamili jioni kwenye ofizi za TFF. Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni Agosti 20 mwaka huu. Fomu kwa nafasi ya Rais ni sh. 500,000, Makamu wa Rais ni sh. 300,000 wakati wajumbe ni sh. 200,000.
Mbwezeleni amesema kwa wale ambao walilipia fomu katika mchakato uliofutwa na wanakusudia kugombea nafasi zilezile walizolipia, hawatalipia tena ada ya fomu husika bali watatakiwa kuambatanisha risiti za malipo wakati wa kurudisha fomu za maombi hayo ili kuthibitisha malipo yao.
Kwa upande wa uchaguzi wa TPL Board, fomu zitaanza kutolewa Agosti 16 hadi 20 mwaka huu, na nafasi zinazogombewa ni Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti ambapo ada ni sh. 200,000 wakati wajumbe wa Bodi ada ni sh. 100,000
|
Na.
|
TAREHE
|
SHUGHULI
|
1.
|
14/08/2013
|
Kamati ya Uchaguzi ya TFF
kutangaza Uchaguzi wa TFF, nafasi za kugombea na sifa za kugombea uongozi wa
TFF.
|
2.
|
16/08/2013
– 20/08/2013
|
Kuchukua Fomu za maombi ya
uongozi wa TFF kutoka kwa Katibu wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF (Katibu Mkuu wa
TFF). Fomu zitatolewa kuanzia saa 3.00 Asubuhi hadi saa 10.00 Alasiri. Mwisho
wa kurudisha fomu kwa Katibu Mkuu wa TFF ni Jumanne tarehe 20/08/2013 saa
10:00 Alasiri.
|
3.
|
21-23/08/2013
|
Kamati ya Uchaguzi ya TFF
kupitia fomu za waombaji uongozi wa TFF. Kutangaza matokeo ya upitiaji fomu
na kuweka wazi kwenye mbao za matangazo majina ya waombaji uongozi wa TFF
(23/08/2013).
|
4.
|
24-26/08/2013
|
Kutoa fursa ya pingamizi kwa
waombaji uongozi. Mwisho wa kupokea pingamizi ni tarehe 26/01/2013 saa 10:00
Alasiri. Pingamizi ziwasilishwe kwa Katibu Mkuu wa TFF. Pingamizi zizingatie
matakwa ya Ibara ya 11(3) ya Kanuni za Uchaguzi.
|
5.
|
27/08/2013
– 29/08/2013
|
Wawekaji Pingamizi na
waliowekewa Pingamizi kuitwa mbele ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF kutoa utetezi
wao kuhusu Pingamizi. Kamati kujadili Pingamizi.
|
6.
|
30/08/2013
- 03/09/2013
|
Usaili na kutangaza matokeo
ya pingamizi na ya usaili / Kuwajulisha kwa maandishi wagombea matokeo ya
usaili. Kutangaza orodha ya awali ya wagombea.
|
7.
|
04
– 06/09/2013
|
Kamati ya Uchaguzi kupitia
Sekretarieti ya TFF kuwasilisha kwenye Kamati ya Maadili ya TFF mashauri yote
ya maadili, kwa kujadiliwa na kutolewa maamuzi na Kamati ya Maadili ya TFF.
|
8.
|
04
– 06/09/2013
|
Kutoa fursa ya kukata Rufaa
kwenye Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF (TFF Elections Appeal Committee) kwa
masuala yasiyo ya Maadili. Rufaa zilizoambatanishwa na ada ya malipo ya Rufaa
zitapokelewa na Katibu Mkuu wa TFF. Mwisho wa kupokea Rufaa ni tarehe 06/09/2013
saa 10:00 Alasiri.
|
9.
|
07-13/09/2013
|
Kamati ya Maadili ya TFF
kupitia mashauri yote yanayohusu Maadili na kuyatolea uamuzi.
|
10.
|
14-
16/09/2013
|
Kamati ya Maadili ya TFF
kutoa matokeo ya maamuzi ya mashauri ya Maadili kwa Kamati ya
Uchaguzi ya TFF na wagombea.
|
11.
|
17-
19/09/2013
|
Kukata Rufaa kwenye Kamati ya
Rufaa ya Maadili ya TFF. Mwisho wa kupokea Rufaa ni tarehe 19/09/2013 saa
10:00 Alasiri.
|
12.
|
20-
24/09/2013
|
Kusikiliza Rufaa
zilizopelekwa kwenye Kamati ya Rufaa ya Maadili ya TFF na kutolea uamuzi.
|
13.
|
25-27
/09/2013
|
Kamati ya Rufaa ya Maadili ya
TFF kuwafahamisha Kamati ya Uchaguzi ya TFF na Wagombea matokeo ya Rufaa zilizosikilizwa
na Kamati ya Rufaa ya Maadili.
|
14.
|
28/09/2013-
02/10/2013
|
Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi
ya TFF kusikiliza Rufaa za Uchaguzi kwa masuala yasiyo ya Maadili.
|
15.
|
03-04/10/2013
|
Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya
TFF kutangaza na kuwapa taarifa za matokeo ya rufaa wagombea waliokata rufaa (zisizohusu
mashauri ya Maadili). Aidha Kamati ya
Uchaguzi ya TFF nayo kufahamishwa matokeo ya rufaa hizo.
|
16.
|
05/10/2013
|
Kutoa orodha ya wagombea wote
waliopitishwa
|
17.
|
06/10/2013-
19/10/2013
|
Kipindi cha Kampeni kwa
wagombea wote.
|
18.
|
20/10/2013
|
Uchaguzi wa Viongozi wa TFF.
|
TANGAZO
UCHAGUZI WA VIONGOZI WA SHIRIKISHO LA MPIRA WA
MIGUU TANZANIA
(TFF)
14/08/2013
1.
Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) inawatangazia wananchi wote kuwa Uchaguzi wa viongozi wa TFF
utafanyika tarehe 20/10/2013 jijini Dar
es salaam . Wale wote wanaopenda kuwania nafasi za
uongozi wa TFF wanataarifiwa kuwa fomu
za maombi ya uongozi wa TFF zitatolewa kuanzia tarehe 16 Agosti 2013 hadi
tarehe 20 Agosti 2013 katika Ofisi ya
Katibu Mkuu wa TFF (Idara ya Fedha),
kuanzia saa 03:00 asubuhi hadi saa 10:00 Alasiri. Mwisho wa kurudisha Fomu ni
saa 10:00 Alasiri tarehe 20 Agosti 2013.
2.
Nafasi zinazotangazwa kugombewa ni:
(i)
Rais wa TFF.
(ii)
Makamu wa Rais wa TFF.
(iii)
Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, nafasi kumi
na tatu (13).
3.
Mtu yeyote
anayeomba nafasi ya uongozi katika TFF lazima atimize masharti yafuatayo:
(i)
Awe Raia wa Tanzania .
(ii)
Awe na kiwango cha elimu kisichopungua Kidato cha
Nne na cheti cha kuhitimu Elimu ya Sekondari.
(iii)
Awe na uzoefu wa uendeshaji wa Mpira wa Miguu
uliothibitishwa wa angalau miaka mitano (5).
(iv)
Asiwe na hatia yoyote ya kosa la jinai na
kuhukumiwa kifungo bila ya uchaguzi wa faini.
(v)
Awe na umri wa angalau miaka 25.
(vi)
Awe amewahi kuwa ama mchezaji Mpira wa Miguu, Kocha,
Mwamuzi au kushiriki katika uendeshaji wa Mpira wa Miguu katika ngazi ya Taifa,
Mkoa, Ligi Kuu au Ligi Daraja la Kwanza .
(vii)
Awe mwadilifu, mwaminifu na mwenye uwezo wa
kutekeleza majukumu, wajibu na malengo ya TFF kwa weledi.
(viii)
Mtu anayegombea nafasi ya Rais na Makamu wa Rais wa
TFF lazima awe na kiwango cha Elimu kisichopungua Shahada ya Chuo Kikuu na awe
na uwezo na haiba ya kuwakilisha TFF ndani na nje ya nchi.
4.
Ada za Fomu za maombi ya
uongozi ni hizi zifuatazo:
(i)
Rais wa TFF; Shillingi Laki Tano (Tshs. 500,000/=).
(ii)
Makamu wa Rais wa TFF; Shillingi Laki Tatu (Tshs.
300,000/=).
(iii)
Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF; Shillingi
Laki Mbili (Tshs. 200,000/=).
5.
Kwa wale ambao walilipia fomu za kugombea katika
mchakato uliofutwa na ambao wanakusudia kugombea nafasi zile zile
walizozilipia, hawatalipia tena ada ya fomu husika bali watatakiwa
kuambatanisha risiti za malipo wakati wa kurudisha fomu za maombi hayo ili
kuthibitisha malipo yao.
6.
Ratiba ya mchakato wa Uchaguzi wa TFF imeainishwa
hapa chini:
7.
Uchaguzi wa TFF unafanyika kwa mujibu wa Katiba ya
TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF.
Hamidu Mbwezeleni
MWENYEKITI
No comments:
Post a Comment