Milan,
Italia
MSHAMBULIAJI
wa Juventus, Carlos Tevez, ametangaza kustaafu rasmi soka la kimataifa.
Nyota
huyo raia wa Argentina aliyetua Juventus majira haya ya joto akitokea Man City,
alisema: "Imefika mwisho.
“Sina
la kuongeza zaidi, nimesema kile ambacho ninajisikia kukieleza, na huo ndiyo
mwisho wa shughuli hiyo. Kama nitasema lingine zaidi ya hilo, nitaonekana kama
ninaomba kuitwa tena. Upande wa Kimataifa ulikuwa wakati uliopita.”
Ancelotti:
Kipa namba moja Real bado
Madrid:
KOCHA wa Real Madrid, Carlo Ancelotti,
amesema bado hajafanya uamuzi wa kipa atakayekuwa chaguo lake la kwanza katika
kikosi chake.
Licha
ya Ancelotti kumchezesha Iker Casillas
katika ushindi wa mabao 3-1 Real iliyoupata dhidi ya Chelsea juzi,
alisema: "Kipindi cha pili, Casillas aliokoa michomo mingi, lakini bado
sijachagua kipa namba moja kwa sababu Jumamosi nitamchezesha Diego López na
baada ya hapo nitaamua."
Zaha
anukia kuitwa England
London: WINGA wa Manchester United, Wilfried Zaha, jana alikuwa
akitarajiwa kuitwa katika Kikosi cha Wakubwa cha England.
Gazeti
la The Daily Mail, lilieleza kuwa kiwango anachokionesha Zaha katika mechi za
kujiandaa na msimu mpya kilitarajiwa kumshawishi Roy Hodgson kumuita kwa ajili
ya kujiandaa na mechi dhidi ya Scotland Jumanne.
Barca
yatolewa 'nduki' kwa Luiz
London:
Chelsea imeitoa 'nduki' Barcelona, baada ya kuiambia kuwa haipo
tayari kupokea ofa yao ya pauni milioni 34.5 (Sh. bilioni 83.8 za Tanzania) kwa
ajili ya kumuuza David Luiz, huku ikiiambia kuwa kamwe isirudi tena kwa kuwa
beki huyo wa kati hauzwi.
Sportsmail
limeeleza kuwa, Luiz alikuwa chaguo la kwanza katika usajili wa beki wa kati
kwa miamba hiyo ya Catalan, lakini Jose Mourinho na uongozi wa Stamford
Bridge umeiambia Barca wala isihangaike
kuongeza ofa yao kwa kuwa Mbrazil huyo hauzwi kwa bei yoyote ile.
No comments:
Post a Comment