Mshambuliaji wa TP Mazembe Mbwana Samatta ameendelea kutikisa nyavu katika michuano ya kombe la shirikisho na kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya FUR Rabat ya Morocco.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Tanzania aliandika bao la pili kunako dakika ya 12 baada ya mshambuliaji raia wa Ghana Solomon Asante kuandika bao la kwanza kwa mabibgwa hao wa soka nchini DR Congo.
Mabingwa hao wa zamani wa Afrika wamejihakikishia alama tatu muhimu katika kundi la B.
Kocha wa Mazembe Patrice Carteron aliaanza mchezo huo kwa kuwatumia washambuliaji wakali wakiwemo akina Tresor Mputu Mabi na Rainford Kalaba.
Samatta mwenye umri wa miaka 21 mpaka sasa ameshafunga jumla ya magoli manne katika michuano hiyo ya kombe la shirikisho akifunga mabao mengine katika michezo ya mchujo kuingia katika kombe la shirikisho baada ya kutolewa katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika.
Samatta alifunga mabao katika michezo yote miwili ya nyumbani na ugenini dhidi ya Liga Muculmana ya Mozambique.
Alifunga goli lingine katika mchezo wa ugenini dhidi ya Entente Setif ya Algeria katika mchezo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1.
No comments:
Post a Comment