MSHAMBULIAJI Wayne Rooney ametangaza ‘bifu’ rasmi na kocha
wake mpya, David Moyes, baada ya kutumia mtandao wake wa kijamii wa Facebook
kumtosa, huku akimshukuru kocha wa timu ya Taifa ya England, Roy Hodgson, kwa imani na msaada anaoonesha
kwake.
Uhasama kati ya Rooney na kocha huyo wa Manchester United
umeongezeka usiku wa kuamkia jana, baada ya mshambuliaji huyo aliyekosa
furaha kutumia ukurasa huo wa Facebook
kutuma ujumbe akimshukuru Hodgson bila
kumzungumzia Moyes.
Kwa
mujibu wa gazeti la Daily Star, katika ujumbe huo mshambuliaji huyo alitoa
salamu nyingi kwa Hodgson bila kutuma shukrani hata moja kwa kocha huyo Old
Trafford. “Shukrani nyingi kwako Roy Hodgson,” ulieleza ujumbe huo ambao
unatafsiriwa ni shukrani za kuungwa mkono na kocha huyo wa timu ya Taifa ya
England katika tatizo la kukwama uhamisho wake kwenye klabu hiyo ya Old Trafford.
Katika
ujumbe huo pia Rooney alimshukuru Hodgson kwa kumchagua kwenye kikosi cha
England ambacho Jumatano kitaivaa Scotland kwenye mechi ya kirafiki, lakini
akashindwa kabisa kumgusia kocha wa klabu kupitia ujumbe huo wa mtandao wa
kijamii.
Mshambuliaji
huyo, ambaye yupo njia panda kuhusu ofa ya pauni milioni 30 iliyotangazwa na
Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho,
anaonekana kuchanganyikiwa zaidi siku za hivi karibuni, baada ya kuonesha wazi
mawazo yake ya kutaka kuondoka.
.Akitoa
shukrani zake zaidi kwa kocha huyo, alisema: “Siwezi kusubiri kujiunga na
kikosi cha England na nina matumaini nitacheza kwa kushinda kama
ilivyo mara zote dhidi ya Scotland.
“Shukrani
nyingi zimwendee Roy Hodgson kwa
kunichagua na kuonesha imani na msaada kwangu,
nalitambua hilo,” aliongeza nyota huyo.
Kauli
hiyo imekuja siku ambayo Rooney ameanza
mazoezi na kikosi cha England kwenye Uwanja wa
Carrington na baadhi ya wachezaji wa kikosi cha wachezaji wenye umri
chini ya miaka 21, kikiongozwa na Nicky Butt, huku akihitaji muda wa wiki
nyingine moja ili aweze kucheza kikosi
cha kwanza.
No comments:
Post a Comment