Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, August 12, 2013

PUSHI MOBILE KUTOA ZAWADI KIBAO FIESTA 2013

Meneja Mauzo na Masoko wa Push Mobile, Rugambo Rodney akimkabidhi funguo mbili Diana Elis Mkoba baada ya kushinda shindano la Tamasha la Serengeti Fiesta 2012. Diana alikabidhiwa magari mawili aina ya Vitz yenye thamani ya shs milioni 18. Katikati ni Baba mdogo wa mshindi, Gratian Mkoba ambaye ni Rais wa chama cha Walimu Tanzania (CWT). Mwaka huu, Kampuni hiyo itatoa magari manne, pikipiki 12nafedhataslim shs 100,000 ikiwa juma ya zawadi zote ni sh million 80. Picha na Mpiga picha wetu.

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Push Mobile Media Limited itatoa zawadi za magari aina ya Vitz manne (4) na pikipiki 12 kwa mashabiki mbali mbali watakaoshinda bahati nasibu maalum ya tamasha la Serengeti Fiesta linalotarajiwa kuzinduliwa Jumamosi mjini Kigoma.

Meneja Masoko na Mauzo wa Push Mobile Media, Rugambo Rodney alisema kuwa zawadi mbali ya magari na pikipiki, pia watatoa zawadi za fedha taslim (sh 100,000) kwa mashabiki hao ambao ili kushinda wanatakiwa kutuma neno Fiesta kwenda namba 15678 ili kuweza kushinda gari, pikipiki au fedha taslim na unaweza kushinda tiketi ya VIP kwa kutuma jina la msanii kwa mfano Diamond na kuacha nafasi na baadaye kuwema maoni yako kwenda namba hiyo hiyo.

Rodney alisema kuwa mbali ya kushinda tiketi, mshiriki atalipiwa tiketi ya ndege kuja Dar es salaam kwa ajili ya kushiriki katika tamasha la fiesta la mwisho. Alisema kuwa wameamua kuweza zawadi hizo nono ili kunogesha zaidi tamasha hilo ambalo kwa kuwanufaisha mashabiki wa muziki hapa nchini.

Aliongeza kuwa wamejipanga ili kuwashirikisha wananchi wote katika tamasha hilo kwani watatoa pia watazindua huduma mpya ijulikanayo kwa jina la Simu TV ambapo itamwezesha mashabiki kuona video mbali mbali za muziki na matukio mengine, kupata nyimbo mbali mbali, kupata taarifa mbali mbali ikiwa pamoja na za michezo kwa kupitia simu ya mkononi.

No comments:

Post a Comment