
Lionel Messi alilazimika kutoka mwishoni mwa kipindi cha
kwanza..baada ya kupata majeraha

Messi akipiga shuti kali jana

ESTADIO VICENTE CALDERON Jana Usiku ilishuhudia
Wachezaji wapya kwa Timu zao wakifunga Bao katika Mechi ya kwanza ya kugombea Supercopa De Espana ambapo Atletico Madrid na Barcelona zilitoka sare Bao 1-1.
Timu hizi zitarudiana huko Nou Camp Jumatano ijayo.
Bao la Atletico Madrid lilifungwa katika Dakika ya 12 na David Villa Mchezaji ambae alihamia Atletico akitokea Barca Mwezi uliopita.

Katika Mechi hii Barca walilazimka kumpumzisha Lionel Messi wakati wa Mapumziko kutokana na maumivu na nafasi yake kuchukuliwa na Cesc Fabregas.

Neymar akisawazisha kwa kichwa na kufanya 1-1

Neymarakishangilia hapa...


David Villa

David Villa ambaye alikuwa wa Barca zamani aliipatia
bao Atletico


Mchezaji wa Atletico Diego Costa akimsukuma Jordi Alba
huku wote wakigombea mpira

kipa Thibaut Courtois na defenders Filipe na Diego Godin
wakimsimamisha Alexis Sanchez

Mario Suarez na Sanchez

Miranda na No 7 Pedro wakikabana.
No comments:
Post a Comment